MTUNGI WA GESI:- Walipuka na Kusababisha Kifo cha Mtu mmoja na Kujeruhi Watu wawili ,wilayani Sengerema mkoni Mwanza. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, May 19, 2014

MTUNGI WA GESI:- Walipuka na Kusababisha Kifo cha Mtu mmoja na Kujeruhi Watu wawili ,wilayani Sengerema mkoni Mwanza.

 ( Tunaomba radhi kwa Picha hii) MWILI WA BWANA JAMES JONH UKIWA UMERUSHA TAKRIBANI MAILI SABINI NA VIUNGO VYAKE VINGINE VIKIWA VIMERUSHA SEHEMU NYINGINE HAPA MIGUU YAKE YOTE IMEKATWA NA KURUSHWA MBALI BAADA YA KULIPUKIWA NA GESI MAY 18,2014.

Picha juu na chini- HII NI NYUMBA AMBAYO IMEHARIBIWA VIBAYA NA MTUNGU WA GESI ULIOLIPUKA NA KUKATIKA VIPENDE VIPANDE NA KWENDA KUANGUKIA NYUMBA HII AMBAYO IMEHARIBIKA VIBAYA LAKINI NDANI YA NYUMA ALIKUWEMO MKE WA BWANA FAYA MATHIAS NA WATOTO WAWILI MMOJA MCHANGA NA MWINGINE MKUBWA ALIEFAHAMIKA KWA JINA LA EVA LAKINI MUNGU ALIMSAIDIA MKE WA WA BWANA MATHIAS KUWEZA KUTOKA  KUPITIA DIRISHANI NA MTOTO MCHANGA LAKINI MTOTO WAKE MWINGINE AMBAE NDIE EVA ALIWEZA KUBAKI NA KUJERUHIWA LAKINI ANAENDELEA VIZURI NA BWANA FAYA AMBAE  YEYE  BADO KALAZWA.


MAREHEMU JAMES JONH ENZI YA UHAI WAKE. TUNAPENDA KUTOA POLE KWA FAMILIA NZIMA YA MAREHEMU JAMES JONH MUNGU AMSAIDIE KATIKA SAFARI YAKE YA UMAUTI.

………..MASHUHUDA WA TUKIO WAKITAZAMA TUKIO LILIVYOTOKEA…………..
MTU MMOJA ALIEFAHAMIKA KWA JINA LA JAMES JONH MKAZI WA SENGEREMA  KATA YA MWABARUHI AMBAE PIA NI DEREVA WA BODABODA APOTEZA MAISHA BAADA YA KULIPUKIWA NA MTUNGI WA GESI. 
 
TUKIO HILI LIMETOKEA  KATIKA ENEO LA ISUNGANG'HORLO KATA YA NYATUKALA MUDA WA SAA TANO ASUBUHI SIKU YA TAREHE 18/05/2014.

CHANZO CHA TUKIO HILO NI PALE BWANA JAMES ALIPOKWENDA KUNUNUA GESI KWA BWANA MMOJA ALIEFAHAMIKA KWA JINA LA FAYA MATHIAS BAADA YA KUFIKA ALIANZA KUHAMISHIWA GESI KUTOKA MTUNGI WA BWANA FAYA MATHIAS KWENDA KATIKA MTUNGI WA NDUGU JAMES JONH  BAADA YA KUKAMILIKA UJAZAJI NDUGU JAMES ALICHUKUA MTUNGI WAKE AKISAIDIANA NA NDUGU FAYA KWENDA KUUFUNGA KATIKA PIKIPIKI YA NDUGU JAMES AKIWA ANAUFUNGA NDIPO ULIPOMLIPUKIA NA KUSABABISHA KIFO CHAKE NA KUMJERUHI NDUGU FAYA NA MTOTO WAKE EVA ALIEKUWA NDANI YA NYUMBA AMBAYO NAYO IMEHARIBIWA VIBAYA.

KITU CHA KUHUZUNISHA NIKWAMBA MWILI WA BWANA JAMES ULISAMBAZWA VIBAYA SANA KITU KILICHOPELEKEA WANANCHI KUANZA KUVIKUSANYA VIUNGO VYAKE SEHEMU TOFAUTI KITU KILICHOPELEKEA SISI TUSIZIWEKE BAADHI YA PICHA ZA VIUNGO VYAKE .

 NDUGU FAYA MATHIAS ALIKIMBIZWA KATIKA HOSPITAL YA WILAYA YA HAPA SENGEREMA AKIWA NA HALI MBAYA SANA LAKINI AKIWA HAJITAMBUI. 

KUNA JAMBO BAYA SANA AMBALO BWANA FAYA JONH AMBAE NDIE MUUZAJI WA GESI MEKUWA AKIFANYA KWA MALA ZOTE NA WATU KUMFUATA WAKIJUA KUWA YEYE NDIE ANAEUZA GESI KWA BEI NAFUU SANA. TUTAWAPA TAARIFA NINI HUWA AKIKIFANYA NA HUENDA NDIO IKAWA CHANZO CHA TATIZO.

Habari/Picha Na:- eaglentertainment Blog.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad