Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya
Muleba mkoani Kagera juzi (May 17, 2014) wameazimia kuigawanya wilaya hiyo kuwa
wilaya mbili ili kurahisisha upatikanaji wa maendeleo ya wananchi ili kujipatia
huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja na utawala wa karibu kwa baadhi ya kata za
mbali na Muleba.
Katibu wa Madiwani wa Chama Cha
Mapinduzi –CCM,wilayani humo Fortunatus Wazia amesema wilaya hiyo kijografia ni
kubwa kwa kuwa na kata 43 na vijiji zaidi ya 160 ambapo upatikanaji wa huduma
za jamii huchelewa.
Wazia amesema katika kuigawa
wilaya hiyo kamati ya madiwani wa CCM inapendekeza ramani iliyochorwa
kugawa wilaya hiyo katika majimbo ya uchaguzi mipaka hiyo itumike kwa
wilaya mpya inayopendekezwa.
Aidha alisema kuwa kisiwa cha Goziba
ambacho kiko mpakani mwa mkoa wa kagera na mwanza kikimilikiwa na wilaya ya
Muleba kiendelee kuwa mkoani kagera badala ya kupelekwa wilaya ya Ukerewe
mkoani Mwanza.
Kauli hiyo imeungwa mkono na kambi
ya upinzani chini ya msemaji wake diwani wa kata ya Kishanda Alfred
Pastory (CUF) ambaye alisema kwa kuzingatia maoni ya wataalamu na jografia ya
wilaya makao makuu ya wilaya mpya pawe kata ya Izigo.
Alitaja sababu za kupendekeza kata
hiyo kuwa makao makuu ya wilaya kuwa ni kuwepo maeneo mapana ya kujenga ofisi
na miundombinu nyingine kuliko kupeleka makao makuu kata ya Kamachumu panapohitaji
kutoa fidia ya ardhi.
Pamoja na maoni hayo baadhi ya
madiwani walivutana katika kupendekeza makao makuu ya wilaya diwani wa
kata ya Kashasha Jonathan Manwah alipendekeza Kamachumu iwe jina la wilaya mpya
na makao makuu kwa kuzingati maoni ya wataalamu pawe izigo kauli iliyoungwa
mkono na madiwani walio wengi.
Hata hivyo Makamu Mwenyekiti wa halmashauri
ya wilaya hiyo Alhaji Swaibu Mfuruki na Mkuu wa wilaya ya Muleba Lambris Kipuyo
waliwataka madiwani hao kuhakikisha wanashirikiana na wananchi pamoja na
serikali kuhimiza maendeleo hasa
upatikanaji wa huduma za jamii.
Habari Na:-Shaaban Ndyamukama- MULEBA.
No comments:
Post a Comment