UBINGWA 2013/2014:- Bayen Munich waunga na Mashabiki wao kusherekea Makombe yao mawili ya Msimu. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, May 19, 2014

UBINGWA 2013/2014:- Bayen Munich waunga na Mashabiki wao kusherekea Makombe yao mawili ya Msimu.

Aidha bao za Arjen Robben na Thomas Muller ndani ya Kipindi cha Pili cha Dakika za Nyongeza 30, baada Mechi kumalizika 0-0, zimewapa Bayen Munich Kombe la Ujerumani, 2014 DFB-Pokal, kwa kuifunga Borussia Dortmund Bao 2-0 kwenye Fainali iliyochezwa Olympiastadion huko Berlin.

Bayern Munich wametwaa Ubingwa wa Bundesliga msimu wa 2013/2014 kwa mara ya 24 huku wakiwa na Mechi 7 ,Huu ni Msimu wa kwanza wa Kocha wao Pep Guardiola kuchukua Ubingwa wa Ligi hiyo.


Kwenye Mechi hii inayokutanisha Vigogo wa Germany ambao walimaliza Bundesliga kwa Bayern kuwa Bingwa na Dortmund kushika Nafasi ya Pili, na inayobatizwa'Der Klassiker', Dortmund walifunga Bao Safi katika Kipindi cha Pili baada Frikiki ya Nuri Sahin kuunganishwa kwa Kichwa na Mats Hummels na Mpira kuonekana kuvuka Mstari wa Golini lakini Refa hakutoa Bao hilo.

Hadi Dakika 90, Bao zilikuwa 0-0 na zikaja Dakika za Nyongeza 30 na Bayern kufunga Bao zao Dakika ya 107 kupitia Robben na Dakika ya 120 kwa Bao la Muller.


Msimu huu, Dortmund imeifunga Bayern mara mbili kwa kuichapa Bayern 4-2 kwenye Fainali ya German Super Cup hapo Tarehe 27 Julai 2013 na  Bayern kuifumua Dortmund 3-0 kwenye Bundesliga hapo Tarehe 23 Novemba 2013 kwenye Mechi iliyochezwa Signal Iduna Park, Nyumbani kwa Dortmund.





No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad