Kwenye
mlipuko huo wa awali uliotokea Jumatatu iliyopita, mhudumu wa nyumba ya kulala
wageni ya kanisa hilo, Benedata Alfred (25) alijeruhiwa na kulazwa katika
Hopitali ya Rufaa ya Bugando.
Kufuatia mlipuko huo, imeelezwa kuwa wakazi wa Mwanza hususan waumini wa kanisa hilo wamekuwa wakiishi kwa hofu kwani wanaamini kuwa aliyekuwa ametega bomu hilo alikuwa na lengo la kuangamiza watu wengi kwa wakati mmoja.
Wakizungumza
na mwandishi wetu kwa sharti la kutochorwa majina yao gazetini, wakazi wa
Makongoro Misheni wamesema hawana imani na mtu aliyetega bomu hilo kama atakuwa
na lengo la kutimiza azima yake aliyokuwa ameipanga au atashindwa kutokana na
ulinzi mkali wa jeshi la polisi ulioimarishwa.
“Tunaishi
kwa mashakamashaka maana hatujui aliyetega bomu lile alikuwa na lengo gani
kwetu, kitendo cha kulitega bomu hilo kanisani kinaashiria mtu huyo alikuwa na
lengo wa kuangamiza watu wengi kwa wakati mmoja,” alisema mmoja wa wakazi hao.
Aidha,
mwingine aliomba jeshi la polisi kuendesha msako mkali kuhakikisha mtuhumiwa wa
bomu hilo anakamatwa na kufikishwa katika mkono wa sheria.
“Tunaomba
polisi watusaidie kuendesha msako mkali ili mtuhumiwa apatikane na kufikishwa
mahakamani ili na sisi tuwe na imani ya kuabudu,” alisema.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Valentino Mlowola alisema uchunguzi wa awali
unaonesha bomu hilo lilitengenezwa kienyeji na uchunguzi unaendelea ili kuwabaini
walioliweka kanisani hapo.
Habari Na:-Global Publishers.
No comments:
Post a Comment