EPL 2013/2014:- Jibu limepatikana na Ubingwa umekwenda Jiji la Manchester badala ya Liverpool. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, May 11, 2014

EPL 2013/2014:- Jibu limepatikana na Ubingwa umekwenda Jiji la Manchester badala ya Liverpool.

Manchester City wamechukua Ubingwa wa Ligi kuu Soka Uingereza Msimu wa 2013/2014 -leo May 11, 2014, mara mbili ndani ya misimu mitatu, mara ya mwisho walikuwa mabingwa msimu we 2011-12…Msimu uliofuata wa 2012-13, majirani zao Manchester United wakalibeba lakini msimu huu wakawa nyanya na Man City wameendelea kulibakiza jijini Manchester.

Man City imebeba kombe hilo baada ya kuitwanga West Ham kwa mabao 2-0 huku Liverpool nao wakishinda kwa 2-1 dhidi ya Newcastle huku Mabao ya City yalifungwa na Samir Nasri na nahodha Vincent Kompany wakati Liverpool walianza kwa Skirtel kujifunga kabla ya Daniel Agger na Daniel Sturridge kusawazisha na kuongeza….Liverpool wameshindwa kuifikia Man City kwa pointi 2, walichokuwa wanaomba leo ni  Man City kupoteza na wao washinde, ili watwae Ubingwa kwa mara ya kwanza baada ya Miaka 24.

Chelsea imemaliza katika nafasi ya tatu baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Cardiff City kwa mabao yaakifungwa na  Schurrle dakika ya 72 na Torres dakika ya 75, huku bao la wapinzani wao likifungwa na Bellamy dakika ya 15.

Arsenal imemaiza katika nafasi ya nne kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya Norwich City, mabao ya Ramsey dakika ya 53 na Jenkinson dakika ya 62. 

Everton iliyoifunga 2-0 Hull City imemaliza katika nafasi ya tano, wakati Tottenham Hotspur imemaliza ya sita baada ya kuifunga 3-0 Aston Villa na Manchester United iliyotoa sare ya 1-1 na Southampton  imemaliza ya saba.

Cardiff 1 - 2 Chelsea 
Fulham 2 - 2 Crystal Palace
Hull 0 - 2 Everton 
Liverpool 2 - 1 Newcastle
Man City 2 - 0 West Ham
Norwich 0 - 2 Arsenal
Southampton 1 - 1 Man Utd
Sunderland 1 - 3 Swansea
Tottenham 3 - 0 Aston Villa
West Brom 1 - 2 Stoke
Kama ilivyo ada, Bingwa wa Ligi Kuu Uingereza na timu tatu za chini yake watacheza Ligi ya Mabingwa barani Ulaya msimu wa 2014/2015, wakati wa tano na sita watakwenda Europa League.

League Table EPL 2013/2014.

Position Team Played Goal Difference Points
1 Man City 38 65 86
2 Liverpool 38 51 84
3 Chelsea 38 44 82
4 Arsenal 38 27 79
5 Everton 38 22 72
6 Tottenham 38 4 69
7 Man Utd 38 21 64
8 Southampton 38 8 56
9 Stoke 38 -7 50
10 Newcastle 38 -16 49
11 Crystal Palace 38 -15 45
12 Swansea 38 0 42
13 West Ham 38 -11 40
14 Sunderland 38 -19 38
15 Aston Villa 38 -22 38
16 Hull 38 -15 37
17 West Brom 38 -16 36
18 Norwich 38 -34 33
19 Fulham 38 -45 32
20 Cardiff 38 -42 30

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad