Orange CAF U-20 - Senegal 2015:- Ngorongoro Heroes ngoma ngumu baada ya kufungwa mabao 2-0 na Nigeria Uwanja wa Taifa-May,11,2014. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, May 11, 2014

Orange CAF U-20 - Senegal 2015:- Ngorongoro Heroes ngoma ngumu baada ya kufungwa mabao 2-0 na Nigeria Uwanja wa Taifa-May,11,2014.

Mshambuliaji wa Ngorongoro, Iddi Seleman (kulia) akimtoka beki wa Nigeria, Ndidi Onyinye, wakati wa mchezo huo uwanja wa Taifa May 11,2014, Ngorongoro itatakiwa kushinda mabao 3-0 ugenini Mei 23,2014 ili kusonga mbele, au ishinde 2-0 na mshindi wa jumla aamuliwe kwa mikwaju ya penalti baada ya kufungwa bao 2-0 nyumbani.

Mshambuliaji wa Ngorongoro Heroes, Saad Kipanga, akiwania mpira na beki wa Nigeria, Omego Izuchukwu, wakati wa mchezo wa kuwania tiketi ya kucheza michuano ya Afrika kwa timu za chini ya Umri wa miaka 20 ambapo Fainali za Mashindano haya zitachezwa Nchini Senegal kuanzia Machi 8 hadi 22 Mwaka 2015 na Timu zitakazotinga Nusu Fainali zitaiwakilisha Afrika kwenye Kombe la Dunia, 2015 FIFA U-20 World Cup, huko Nchini New Zealand.


Nchi 28 za Afrika zimeshiriki Raundi ya Mtoano ya Mashindano ya CAF kwa Vijana wa chni ya Miaka 20, Orange CAF U-20 Africa Youth Championship Senegal 2015, na Tanzania, ikiwa na Timu yake Ngorongoro Heroes, ikicheza Jumapili (May 11, 2014) Jijini Dar es Salaam na Nigeria wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 na kuondosha matumaini ya Ngorongoro kushinda katika mchezo wa marudiano unaotarajia kuchezwa Nigeria. 

Ngorongoro Heroes katika mchezo wa marudiano wana kibarua kigumu kwani Nigeria ndio wenye Rekodi kwenye michuano hii kwa kutwaa Kombe hili mara 6 wakifuatiwa na Egypt waliolitwaa mara 4.

Kipa wa pili, Peter Manyika Peter alifungwa bao la kwanza dakika ya tano tu tangu aingie na Yahya Musa, aliyemalizia krosi ya chinichini ya Muhamed Musa dakika ya 50.
Nigeria walifanya shambulizi la kushitukiza na kufanikiwa kupata bao la pili, lililoinyong’onyesha kabisa Tanzania kupitia kwa mchezaji wao Awoinyi Taiwo baada ya kutumia vizuri makosa ya beki Pato Ngonyani aliyechelewa kuondosha mpira kwenye eneo la hatari.     

Kwa matokeo hayo, Ngorongoro itatakiwa kushinda mabao 3-0 ugenini Mei 23 ili kusonga mbele, au ishinde 2-0 na mshindi wa jumla aamuliwe kwa mikwaju ya penalti.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad