MKESHA WA MWENGE 2014:-Ilikuwa ni Full Burudani-May 08 kuamkia May 09,2014-katika Viwanja vya Posta ya zamani Mjini Ngara. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, May 11, 2014

MKESHA WA MWENGE 2014:-Ilikuwa ni Full Burudani-May 08 kuamkia May 09,2014-katika Viwanja vya Posta ya zamani Mjini Ngara.

Ni umati wa wakazi mbalimbali wa wilaya ya Ngara mkoani Kagera wakiwa wamekusanyika kwenye uwanja wa Posta ya zamani mjini Ngara ambako Mwenge wa Uhuru 2014 ulikesha hapo May 08 kuamkia May 09,2014,ikiwa ni miaka 14 toka ulipokesha mwaka 2000.


Pamoja na  kuzindua, Kukagua,Kufungua na Kuweka mawe ya msingi miradi saba yenye thamani ya shilingi Bilioni 1 .2  katika miradi ya Maendeleo na Mwenge huo, Mkuu wa wilaya ya Ngara Bw Kanyasu aliwaongoza wanangara Kukesha pamoja huku burudani mbalimbali zikichombeza mkesha huo.



Nao watalaamu wa Afya toka Idara ya Afya wilaya ya Ngara ,mkoani Kagera walikutwa na Camera yetu wakifanya yao kwa kuhakikisha Wananchi mbalimbali waliojitokeza kwa hiari yao wanajua Afya zao kwa Kupimwa damu ili kujua kama wana maambuziki ama la...


.......Bada la Idara ya Afya wilaya ya Ngara katika Viwanja vya Posta ya zamani likiwa limejaa wananchi waliojitokeza kwa hiari yao kupima afya......siku ya Mkesha wa Mwenge wa Uhuru 2014-May 08.

Aidha baada ya kumaliza mbio zake Mkoani Kagera ,Asubuhi ya May 10, 2014-Mwenge wa Uhuru sasa uko Mkoani Kigoma kuendelea na Mbio zake na JUMLA ya miradi 62 ya maendeleo inayofikia thamani ya Zaidi Bilioni 10.7 inatarajiwa kuzindiliwa, kukaguliwa na kuwekewa mawe ya msingi katika mbio za mwenge zilizoanza Jumamosi (May 10, 2014)  ukianzia wilaya ya Kakonko ambapo itapitia katika Halmashauri saba za wilaya sita katika mkoa Kigoma.

Mwenge huo unatarajia kuitimisha mbio zake Oktoba 14 ,2014,mkoani Tabora, ambapo zinatarajia kufungwa na mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete.
 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad