Utafiti
uliofanywa na Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini umeonyesha asilimia 20 ya
saratani ya koo husababishwa na ngono ya mdomo maarufu kama ‘Oral Sex”.
Utafiti huo
unaonyesha saratani ya koo licha ya kuambukizwa na njia mbalimbali ikiwemo
ulaji wa vyakula vyenye pilipili, pombe
kali, vitu vyenye uchachu pamoja na kurithi kutoka kwa wazazi.
Utafiti
unaonyesha watu wengi hasa vijana wanamejiingiza kwenye vitendo hivi vya
kufanya ngono wakitumia midomo hasa ndimi, hivyo kuhatarisha uhai wao.
Katika
utafiti huo wa hivi karibuni, ulibaini wanaume 747 na wanawake
wakiwa 472 hugundulika kila mwaka kuwa na saratani hiyo huku wanaopoteza maisha
kila mwaka ni wanaume 444 wakifuatiwa na wanawake 270 kutokana na ugonjwa huo.
Utafiti
unabainisha kuwa asilimia kubwa ya vijana wenye umri kati ya miaka 20 hadi 45
wanatumia staili ya kuwanyonya wenza wao sehemu za siri lengo likiwa ni
kuwavutia wapenzi wao katika kushiriki ngono.
Vijana
wenye umri huo ndio wahanga wakubwa kwa sasa kutokana na ugonjwa huo kuonekana
kuwaathiri kwa kasi, huku wengi wakiwa hawajui athari zake.
Baadhi hujisifia
kwamba ni wajuzi, kumbe wanajitafutia kifo kwa kufanya vitendo hivyo.
Utafiti
unaonyesha kwa watu wazima walio wengi hawana muda wa kufanya hayo wanayofanya
vijana, hivyo kujikuta angalau wanakuwa salama na kupatwa na saratani ya koo
kwa njia hiyo inayoonekana kama ni chafu pia.






No comments:
Post a Comment