Picha za Mechi ya Simba SC na Mtibwa Sugar huko Morogoro, kwenye Mechi ya Ligi Kuu Vodacom na kutoka Sare ya Bao 1-1. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, February 06, 2014

Picha za Mechi ya Simba SC na Mtibwa Sugar huko Morogoro, kwenye Mechi ya Ligi Kuu Vodacom na kutoka Sare ya Bao 1-1.


Kikosi cha Timu ya Soka ya Mtibwa Nyuma kuanzia Kushoto:JumaLuizio,Shaban Nditi, Hassan Ramadhan,Ally Shomary  Salim Mbonde.Mbele Kuanzia Kushoto : Jamal Mnyate,Said Mkopi,Shaban Kisiga, Husein Sharif,Salvatory Mtebe,Mussa Mgosi.

Kikosi cha Timu ya Soka ya Simba Kilichoanza Dhidi ya Mtibwa leo(Februari 05,2014).
Nyuma Kuanzia Kushoto: Kocha Msaidizi Seleman Matola,Tambwe,Amri Kiemba,Joseph Owino,Jonas Mkude,Musoti.Mbele Kushoto:Singano,Awadhi,Haruna Chanongo,Ivo Mapunda,Rashid Baba Ubaya,Haruna Shamte.

Waamuzi wa Mchezo wa Leo wakiwa na Manaodha wa Timu Zote Mbili.
 

Mashabiki waliojitokeza katika Mchezo huo wakishangilia muda wote wa Mchezo.

Golikipa wa Timu ya Mtibwa Sugar Hussein Sharif Akiwa Ameokoa Moja ya Purukushani katika Lango Lake.Akishihudiwa na Beki wake Salim Mbonde Pamoja na Mshambuliaji wa Simba Khamisi Tambwe.

Mashabiki waliojitokeza katika Mchezo huo wakishangilia muda wote wa Mchezo.
 

Wachezaji wa Timu ya Soka ya Mtibwa Sugar Wkishanilia Goli Lililofungwa na Musa Mgosi  Katika Dakika ya 18 ya Mchezo.
 
Mashabiki waliojitokeza katika Mchezo huo wakishangilia muda wote wa Mchezo.
Simba SC imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Mtibwa Sugar iliyomaliza pungufu ya mchezaji mmoja baada ya Nahodha wake, Shaaban Nditi kuonyeshwa kadi nyekundu kipindi cha pili katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Matokeo haya yamewanufaisha kidogo Simba SC  kwa kufungana kwa Pointi na Mbeya City lakini wao kukamata Nafasi ya 3 kwa ubora wa Magoli na sasa wako Pointi 4 nyuma ya Yanga walio Nafasi ya Pili na 5 nyuma ya Vinara Azam FC.

NO
TEAMS
P
W
D
L
GF
GA
GD
PTS
1
Azam FC
16
10
6
0
29
10
19
36
2
Young Africans
16
10
5
1
34
12
22
35
3
Simba SC
16
8
7
1
33
14
19
31
4
Mbeya City
16
8
7
1
22
13
9
31
5
Mtibwa Sugar
16
5
7
4
20
19
1
22
6
Kagera Sugar
16
5
6
5
15
15
0
21
7
Coastal Union
16
3
10
3
11
8
3
19
8
Ruvu Shootings
14
4
6
4
16
16
0
18
9
JKT Ruvu
15
6
0
9
13
19
-6
18
10
Ashanti United
16
3
4
9
14
28
-14
13
11
Rhino Rangers
16
2
6
8
11
20
-9
12
12
JKT Oljoro
16
2
6
8
12
17
-5
12
13
Tanzania Prisons
14
1
7
6
6
16
-10
10
14
Mgambo JKT
15
2
3
10
7
26
-19
9

Katika Mechi nyingine za VPL zilizochezwa Feb 05,2014, huko Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya, Tanzania Prisons na Coastal Union zilitoka Sare ya 0-0, na Ashanti United ikicheza Ugenini Uwanja wa Azam Complex iliifunga JKT Ruvu Bao 1-0 wakati Rhino Rangers na JKT Oljoro, zikicheza huko Tabora, zilitoka Sare ya Bao 2-2.

 RATIBA MECHI ZIJAZO.

Jumapili Februari 9,2014.

JKT Oljoro v Kagera Sugar

Rhino Rangers v Coastal Union

Mbeya City v Mtibwa Sugar

JKT Ruvu v Ruvu Shooting

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad