 |
Rais Jakaya
Kikwete.**Jumla ya Watanzania 438,726 walipiga kura kupendekeza majina
mbalimbali. Watu 10 waling’ara zaidi kwa kugawana jumla ya kura asilimia 97.4,
huku wengine ambao hawakuweza kuchomoza wakiambulia mgawo wa asilimia 2.6.
|
Katika hao
10 waliong’ara zaidi, mtiririko kulingana na wingi wa kura unagawanywa kama…
Kwa muda wa
miezi miwili , magazeti ya Global Publishers Ltd yaliendesha zoezi la
kuwashirikisha wasomaji wake juu ya mtu gani mwenye nguvu zaidi ya ushawishi
katika jamii ya Watanzania.
Dk. Jakaya
Mrisho Kikwete.
Rais Jakaya
Mrisho Kikwete anashika nafasi ya kwanza.
Kwa nafasi yake kama mkuu wa nchi,
Amiri Jeshi Mkuu wa vikosi vyote vya ulinzi na usalama, Mwenyekiti wa Baraza la
Mawaziri na Mwenyekiti wa Chama Tawala CCM, ndiye aliyeongoza kwa kupata kura
nyingi kwamba ana ushawishi mkubwa katika makundi yote. Watu 118,456 ambao ni
sawa na asilimia 27 walimchagua.
 |
Edward
Ngoyai Lowassa.**Waziri Mkuu wa zamani, Edward Ngoyai Lowassa anashika nafasi
ya pili kwa nguvu ya ushawishi katika Tanzania. Ingawa hayumo kwenye Baraza la
Mawaziri, ameonesha anakubalika sana kijamii kwa kuchaguliwa na watu 83,358
ambao ni sawa na asilimia 19.
|
 |
Zitto Zuberi
Kabwe.**Mbunge huyu wa Kigoma Kaskazini Chadema ndiye alifungua milango kwa
vijana wengi kujiingiza katika siasa mwaka 2005.
Umahiri wake katika kujenga
hoja zinazotikisa nchi, zilimpatia umaarufu mkubwa ndani na nje ya chama chake.
Anachukuliwa kama kijana aliyewapa wenzake uwezo wa kujiamini.
Pamoja na
misukosuko ya kisiasa inayomkabili lakibi bado ameng’ara kwa kuchaguliwa na
watu 65,809, sawa na aslimia 15.
|
 |
Reginald
Abraham Mengi.**NI mfanyabiashara mkubwa mzawa, maarufu pengine kuliko wote
Tanzania.
Ndiye mtu anayemiliki vyombo vingi vya habari, vikiwemo televisheni,
redio na magazeti.
Ni mmoja wa matajiri wachache wenye utamaduni wa kuwasaidia
wasiojiweza. Kutokana na mchango wake kijamii, naye ameng’ara. Watu 43,873
ambao ni sawa na asilimia 10 walimchagua.
|
 |
Kadinali
Polycarp Pengo.**MUADHAMA Polycarp Kardinali Pengo ni kiongozi wa madhehebu ya
Kikatoliki anayeheshimika katika jamii ya Kitanzania.
Ni mtu makini na
anayehubiri amani na upendo muda wote. Taswira yake kwenye jamii imemuwezesha
kuchaguliwa na watu 35,098 (asilimia 8).
|
 |
Dk.
Willibroad Peter Slaa.**KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema).
Alijipatia umaarufu mkubwa wakati alipokuwa mbunge wa kuchaguliwa
Jimbo la Karatu. Uwezo wake wa kujenga hoja na kuitetea, msimamo mkali dhidi ya
rasilimali za taifa kulimfanya kupendwa na wengi.
Jambo hili
lilimfanya kuwa mpinzani mkubwa wa CCM wakati wa uchaguzi mkuu uliopita, ingawa
baadaye alishindwa na Rais Kikwete. Mvuto wake kwa wananchi, ulichangia pia
kuongezeka kwa idadi ya wabunge wa chama chake, kutoka 11 mwaka 2005 hadi 48.
Watu 26,324 (6%) wamempigia kura.
|
 |
Said Salim
Bakhressa.**MFANYABIASHARA maarufu nchini na mmoja wa watu wanaotajwa kuwa na
fedha nyingi zaidi Tanzania. Anamiliki viwanda vya kutengeneza unga, juisi,
matunda, biskuti, soda na koni. Pia ndiye msambazaji mkubwa wa unga kwa nchi za
Afrika Mashariki na Kati.
Bakhressa
ambaye ni Mzanzibari, pia anamiliki timu ya mpira wa miguu ya Azam FC ambayo ni
ya kwanza nchini kuwa na uwanja wake wa kisasa. Ndiye mmiliki wa kituo cha
televisheni cha Azam TV, vilevile ana vyombo vya usafiri wa majini. Watu 21,936
(5%) wamemchagua.
|
 |
John Pombe
Magufuri.**MMOJA wa mawaziri wenye historia nzuri ya uchapa kazi kiasi cha
kusifiwa sana na wananchi. Tokea alipoibuliwa kwa mara ya kwanza na kuwa waziri
wakati wa utawala wa Awamu ya Tatu, kasi yake imezidi kung’aa na kumfanya kuwa
kipenzi cha wananchi. Katika orodha hii amechaguliwa na watu 17,549 (4%).
|
 |
Dk. Harrison
George Mwakyembe.**Makali yake yalidhihirika zaidi alipoongoza Kamati Teule ya
Bunge iliyochunguza kuhusu uwepo wa ufisadi katika kampuni ya kufua umeme ya
Richmond mwaka 2007-2008, kazi ambayo ilimalizika kwa aliyekuwa Waziri Mkuu
wakati huo, Edward Lowassa kuachia ngazi pamoja na Ibrahim Msabaha na Nazir
Karamagi, waliokuwa mawaziri wakati huo.
Kazi yake
nzuri akiwa mbunge, baadaye kuwa naibu waziri wa Uchukuzi na hata baada ya kuwa
waziri kamili, imemfanya achaguliwe na watu 8,775 (2%) kuwa mmoja wale 10 wenye
ushawishi.
|
 |
Shekhe Issa
Ponda.**Ni Katibu wa Jumuiya za Kiislam Tanzania. Amekuwa akiendesha harakati
nyingi kudai haki za Waislam, hivyo kumfanya awe akilumbana na serikali mara
kwa mara. Anachokifanya kinabeba maana kubwa kwa watu, ndiyo maana amechaguliwa
kwa kura 6,142 (1.4%), hivyo kufunga orodha ya wale 10 wenye mvuto zaidi
Tanzania kwa mwaka 2013-2014.
|
Sorce:-
GLOBAL
No comments:
Post a Comment