Simba SC na ushindi wa 4-0, sasa pointi 30 nyuma ya Mbeya City,Yanga SC na Azam FC katika msimamo wa Ligi Kuu Vodacom Bara. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, February 02, 2014

Simba SC na ushindi wa 4-0, sasa pointi 30 nyuma ya Mbeya City,Yanga SC na Azam FC katika msimamo wa Ligi Kuu Vodacom Bara.

Mshambuliaji wa Simba SC, Amissi Tambwe aliyetupia 'hat trick' dhidi ya JKT Oljoro Jumamosi (Februari 01,2014) na Kuipa Simba SC ushindi wa bao 4-0 katika mtanannge uliopigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.


KIKOSI SIMBA:-Ivo Mapunda, William Lucian, Baba Ubaya, Joseph Owino, Donald Musoti, Jonas Mkude, Haruna Chanongo, Awadhi Juma, Amri Kiemba, Amissi Tambwe na Ramadhan Singano 'Messi'.

JKT OLJORO:- Mohamed Ali, Paul Malipesa, Ali, Omar, Nurdin Mohamed, Sabri Makame, Babu Ally, Jacob Masawe, Amir Omar, Shijja Mkina, Majaliwa Mbaga



'Hat trick' ya Mchezaji kutoka Burundi, Amisi Tambwe, na Bao la Jonas Mkude, leo zimewapa Simba ushindi mnono wa Bao 4-0 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam walipocheza na JKT Oljoro kwenye Mechi ya Ligi Kuu Vodacom Tanzania bara Jumamosi Februari 01,2014.

Hadi Mapumziko Simba SC walikuwa mbele kwa Bao 3-0 yakiwekwa kimiani na Amissi Tambwe aliyetupia 3 wakati lingine likifungwa na Jonas Mkude..

Ushindi huu umewabakiza Simba Nafasi ya 4 baada ya kucheza michezo 15  wakiwa na Pointi 30 zikiwa ni Pointi 1 nyuma ya Mbeya City ambao wako Nafasi ya 3.

Katika Mechi nyingine ya Ligi iliyochezwa , huko Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam kati ya Ashanti United walichapwa Bao 2-0 na Mgambo JKT.

Leo Jumapili Februari 02,2014,Jijini Dar es Salaam zipo Mechi mbili ambapo Vinara wa Ligi Azam FC watakuwa kwao Azam Complex kucheza na Kagera Sugar na Yanga, walio Pointi 1 nyuma ya Azam FC, wapo Uwanja wa Taifa kucheza na Timu ngumu Mbeya City ambao wako Pointi 1 nyuma ya Yanga.

RATIBA MECHI ZIJAZO LIGI KUU VODACOM.

Jumapili Februari 02,2014.

Yanga vs Mbeya City (Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam)

Azam vs Kagera Sugar (Uwanja wa Azam Complex, Chamazi)

Jumatano Februari 05,2014.

Tanzania Prisons vs Coastal Union (Uwanja wa Sokoine, Mbeya)

Mgambo Shooting vs Ruvu Shooting (Uwanja wa Mkwakwani, Tanga)

Rhino Rangers vs Oljoro JKT (Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora)

JKT Ruvu vs Ashanti United (Uwanja wa Azam Complex, Chamazi)


MSIMAMO LIGI KUU VODACOM TANZANIA BARA 2013/2014.

NO
TEAMS
P
W
D
L
GF
GA
GD
PTS
1
Azam FC
15
9
6
0
25
10
15
33
2
Young Africans
15
9
5
1
33
12
21
32
3
Mbeya City
15
8
7
0
22
12
10
31
4
Simba SC
15
8
6
1
31
13
18
30
5
Kagera Sugar
15
5
6
4
15
11
4
21
6
Mtibwa Sugar
15
5
6
4
19
18
1
21
7
Coastal Union
15
3
9
3
11
8
3
18
8
Ruvu Shootings
14
4
6
4
16
16
0
18
9
JKT Ruvu
14
6
0
8
13
18
-5
18
10
Rhino Rangers
15
2
5
8
9
18
-9
11
11
JKT Oljoro
15
2
5
8
10
15
-5
11
12
Ashanti United
15
2
4
9
13
28
-15
10
13
Tanzania Prisons
13
1
6
6
6
16
-10
9
14
Mgambo JKT
15
2
3
10
7
26
-19
9


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad