![]() |
|
RVP: Robin
van Persie (20) akishangilia na wenzake wa Man Utd baada ya kuifungia bao la
kusawazisha dakika ya 47 ya mchezo.
|
![]() |
|
Kocha wa Man
Utd, David Moyes akiwa na machungu baada ya timu yake kupigwa huku wachezaji
wake Jonny Evans na Phil Jones wakiumia ambapo Jones alikimbizwa hospitali.
|
Manchester
United imeendelea kusuasua katika Ligi Kuu ya Uingereza baada ya kupokea
kichapo cha bao 2-1 kutoka kwa Stoke City
jana Jumamosi (Februari 01,2014) ikiwa ni mechi ya nane kupokea vipigo katika
ligi hiyo.
Ushindi huo
wa Stoke City ni wa kwanza kwenye Ligi tangu Mwaka 1984 dhidi ya Man United
Uwanjani Britannica.
Mabao yote
ya Stoke yamefungwa na Charlie Adam katika dakika ya 38 na 52 wakati bao la
Manchester United likifungwa na Robin van Persie dakika ya 47. Kwa matokeo ya
leo, Man Utd imebaki na pointi zake 40.
Katika mechi
ya leo, wachezaji wawili wa Man Utd, Jonny Evans na Phil Jones waliumia ambapo
Jones alikimbizwa hospitali kwa matibabu zaidi baada ya kugongana na Jon
Walters wa Stoke.
Newcastle 0 - 3 Sunderland
West Ham 2 - 0 Swansea
Cardiff 2 - 1 Norwich
Everton 2 - 1 Aston Villa
Fulham 0 - 3 Southampton
Hull 1 - 1 Tottenham
Stoke 2 - 1 Man Utd
| Position | Team | Played | Goal Difference | Points |
|---|---|---|---|---|
|
LIGI KUU UINGEREZA RATIBA MECHI ZIJAZO.
[Saa za Bongo]
Jumapili Februari 2,2014.
16:30 West Brom v Liverpool
19:00 Arsenal v Crystal Palace
Jumatatu Februari 3,2014.
23:00 Man City v Chelsea
| ||||
| 1 | Man City | 23 | 42 | 53 |
| 2 | Arsenal | 23 | 24 | 52 |
| 3 | Chelsea | 23 | 23 | 50 |
| 4 | Liverpool | 23 | 29 | 46 |
| 5 | Everton | 24 | 12 | 45 |
| 6 | Tottenham | 24 | -1 | 44 |
| 7 | Man Utd | 24 | 10 | 40 |
| 8 | Newcastle | 24 | 1 | 37 |
| 9 | Southampton | 24 | 7 | 35 |
| 10 | Aston Villa | 24 | -7 | 27 |
| 11 | Stoke | 24 | -14 | 25 |
| 12 | Swansea | 24 | -6 | 24 |
| 13 | Hull | 24 | -7 | 24 |
| 14 | Sunderland | 24 | -11 | 24 |
| 15 | Norwich | 24 | -18 | 24 |
| 16 | Crystal Palace | 23 | -16 | 23 |
| 17 | West Brom | 23 | -6 | 22 |
| 18 | West Ham | 24 | -9 | 22 |
| 19 | Cardiff | 24 | -22 | 21 |
| 20 | Fulham | 24 | -31 | 19 |
LIGI KUU
SOKA HISPANIA :- LA LIGA.
FC Barcelona
walitangulia kufunga Bao katika Dakika ya 7 Mfungaji akiwa Alexis Sanchez na
Valencia kujibu na kupiga Bao mbili katika Dakika ya 44 lililofungwa na Parejo
na Dakika 4 baadae kupitia Pablo Piatti.
Barca
walisawazisha kwa Penati ya Lionel Messi na hilo ni Bao lake la kwanza baada
kutofunga katika Mechi 3 lakini Paco Alcácer, katika Dakika ya 59, aliipigia
Valencia Bao la 3 na kuwapa ushindi.
Barca
walimaliza wakiwa Mtu 10 baada Jordi Alba kupewa Kadi ya Njano ya pili kwenye
Dakika ya 78 na kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu.
Ukiiondoa
Real Madrid, Valencia imekuwa Timu ya kwanza kuondoka Nou Camp bila kufungwa
tangu Oktoba 2011 Sevilla ilipopata Sare ya 0-0.
Matokeo haya
yameiacha Barca uongozini ikiwa Pointi 54, sawa na Atletico Madrid, lakini
Atletico wana Mechi moja mkononi ambayo watacheza Nyumbani kesho Jumapili na
Real Sociedad wakati Real Madrid, walio Pointi 1 nyuma ya Barca na Atletico,
pia watacheza Jumapili Ugenini na Athletic Bilbao.
Atletico na
Real zina nafasi nzuri kuitungua Barca toka kileleni.
RATIBA/MATOKEO
LA LIGA.
Barcelona 2
- 3 Valencia CF
Levante
0 - 0 Rayo Vallecano
Getafe 0 - 0 Real Valladolid
| Position | Team | Played | Goal Difference | Points |
|---|---|---|---|---|
| 1 | Barcelona | 22 | 43 | 54 |
| 2 | Atlético Madrid | 21 | 38 | 54 |
| 3 | Real Madrid | 21 | 39 | 53 |
| 4 | Athletic Bilbao | 21 | 14 | 42 |
| 5 | Villarreal | 21 | 17 | 37 |
| 6 | Real Sociedad | 21 | 12 | 36 |
| 7 | Sevilla | 21 | 5 | 31 |
| 8 | Valencia CF | 22 | -4 | 28 |
| 9 | Levante | 22 | -8 | 28 |
| 10 | Espanyol | 21 | -2 | 26 |
| 11 | Celta de Vigo | 22 | -6 | 25 |
| 12 | Getafe | 22 | -12 | 25 |
| 13 | Granada CF | 22 | -9 | 24 |
| 14 | Osasuna | 21 | -16 | 22 |
| 15 | AlmerÃa | 21 | -18 | 22 |
| 16 | Málaga | 21 | -8 | 21 |
| 17 | Elche | 21 | -13 | 21 |
| 18 | Real Valladolid | 22 | -13 | 20 |
| 19 | Rayo Vallecano | 22 | -30 | 17 |
| 20 | Real Betis | 21 | -29 | 11 |
RATIBA/MATOKEO
LA LIGA.
Jumapili
Februari 2,2014.
Elche CF v
UD Almeria
Real Betis v
RCD Espanyol
Atletico de
Madrid v Real Sociedad
Athletic de
Bilbao v Real Madrid CF
Jumatatu
Februari 3,2014.
Villarreal CF
v Osasuna










No comments:
Post a Comment