Nusu Fainali za Kombe la Mfalme.:-Real Madrid yaifumua Atletico Madrid Bao 3-0 huku FC Barcelona nae akishinda dhidi ya Real Sociedad. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, February 06, 2014

Nusu Fainali za Kombe la Mfalme.:-Real Madrid yaifumua Atletico Madrid Bao 3-0 huku FC Barcelona nae akishinda dhidi ya Real Sociedad.

Usiku wa jana Feb 05,2014 ni furaha bwelele baada ya Timu yao Real Madrid kuwatandika Wapinzani wao wa Jadi Atletico Madrid Bao 3-0 katika Mechi ya Kwanza ya Nusu Fainali za Kombe la Mfalme, Copa del Rey.

Mechi hii, maarufu huko Jijini Madrid Nchini Spain kama El Derbi madrileño, ilikuwa pia na burudani tosha kwa vitimbwi kati ya Sentahafu wa Real Kepler Laveran Pepe na Fowadi wa Atletico Diego Costa wakifanyiana undava na kutishana huku, kama kawaida yake, Sergio Ramos, akitia chapuo za hapa na pale.
Atletico, ambao ndio Mabingwa Watetezi wa Kombe hili na pia ni Vinara wa La Liga wakiwa Pointi 3 mbele ya Barcelona na Real Madrid zinazofungana kwa Pointi, walitinga kwenye Mechi hii wakiwa na nia ya kujihami kwa kumwacha Diego Costa kuwa Straika pekee. 

Real, ambao walitawala, walikuwa shapu na kuonana sana, walipata Bao la kwanza Dakika ya 17 baada ya Shuti la Pepe kumbabatiza Insua na kutinga.

Bao la Pili la Real, lilikuwa safi sana, kufuatia ushirikiano mzuri na Jese Rodriguez kumalizia kwenye Dakika ya 57.

Bao la Tatu ni la Shuti la Angel Di Maria ambalo lilimbabatiza Joao Miranda na kutingisha kamba kwenye Dakika ya 73.

Timu hizi zitarudiana huko Estadio Vicente Calderon hapo Jumanne Februari 11 na ili Atletico waendelee kulitetea Taji lao inabidi waichape Real Madrid Bao 4-0.

Barcelona 2 v 0 Real Sociedad

COPA del REY
NUSU FAINALI
[Saa za Bongo]
Marudiano
Jumanne Februari 11,2014.

23:00 Atletico de Madrid v Real Madrid CF [0-3] [Estadio Vicente Calderon]

Jumatano Februari 12,2014.

24:00 Real Sociedad v FC Barcelona [Estadio Anoeta]

FAINALI

Aprili 19,2014.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad