|
Katibu wa
umoja wa vijana CCM kata ya Majengo Sebastian Masunga ambaye amekatwa kabisa
mkono wake wa kushoto.
|
|
Dereva wa
CCM Wilaya ya Kahama Charles Peter aliyekatwa mapanga Kichwani.
|
|
Katibu
Mwenezi wa CCM Wilaya ya Kahama Masoud Melimeli ambaye amekatwa kiganja cha
mkono.
|
| Ramadhani Salumu, ambaye ni muhamasishaji wa chama cha Mapinduzi Wilaya ya Kahama. |
![]() |
|
Mbunge wa
Jimbo la Maswa Mashariki, Sylvester Kasulumbayi, anayeshikiliwa na Jeshi la Polisi
wilaya ya Kahama kufuatia vurugu hizo.
|
Wanachama
sita wa CCM akiwemo katibu Mwenezi wa chama hicho wilayani Kahama wamejeruhiwa
vibaya baada ya kukatwa mapanga na kundi la watu wanaodaiwa kuwa wafuasi wa
CHADEMA, katika kata ya Ubagwe Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga.
Tukio hilo
limetokea jana(Februari 05,2014) Majira ya saa moja jioni wakati wafuasi hao wa
CCM wakitoka katika mkutano wa Hadhara wa kumnadi mgombea wa chama hicho katika
uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Ubagwe wilayani Kahama.
Waliojeruhuwa
katika tukio hilo ni katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Kahama Masoud Melimeli
ambaye amekatwa kiganja cha mkono wa kulia na Afisa mtendaji kata ya Ubangwe
Alphonce Kimaro ambaye amekatwa panga usoni.
Wengine ni
katibu wa umoja wa vijana CCM kata ya Majengo Sebastian Masunga ambaye amekatwa
panga kichwani na kukatwa kabisa mkono wake wa kushoto na dereva wa CCM Wilaya
ya Kahama Charles Peter aliyekatwa mapanga Kichwani.
Pia
amejeruhiwa Ramadhani Salumu, ambaye ni muhamasishaji wa chama cha Mapinduzi
aliyejeruhiwa mguuni pamoja na Subira Nyangusu, huku ikielezwa kuwa watuhumiwa
wa tukio hilo walipasua vioo vya gari la CCM na kuchukua funguo za gari hiyo.
Kwa mujibu
wa Mganga Mkuu wilaya ya Kahama, Andrew Emanuel majeruhi hao wamelazwa katika
hospital ya wilaya hiyo, huku Kimaro, Masunga na Peter ambao hali zao ni mbaya
wakipelekwa hospitali ya rufaa ya Bugando jijini Mwanza.
Imedaiwa
katika tukio hilo wafuasi hao wa Chadema wamepora fedha zaidi ya shilingi
milioni moja na laki tatu kutoka kwa watu mbalimbali pamoja na simu za mkononi.
Kamanda wa
Polisi mkoa wa Shinyanga, Evarist Mangala amesema watuhumiwa 16 wa tukio hilo
ambao ni wafuasi wa CHADEMA akiwemo Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki,
Sylvester Kasulumbayi, wanashikiliwa na jeshi la Polisi wilaya ya Kahama.






No comments:
Post a Comment