![]() |
|
Mbunge wa
Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe akiwa ndani ya Mahakama Kuu akisubiri
hukumu ya kesi yake leo(Januari 07,2014).
|
![]() |
|
Mwanasheria
wa Zitto Kabwe, Albert Msando akiwasili Mahakama Kuu kusikiliza hukumu ya
Zitto.
|
![]() |
|
Mwanasheria
wa Chadema, Peter Kibatara (kushoto) akiwa na Mkurugenzi wa Sheria na Haki za
Binadamu wa chama hicho, Tundu Lissu ndani ya Mahakama Kuu tayari kusikiliza
hukumu ya Zitto.…
|
![]() |
|
Tundu Lissu
akitoka mahakamani baada ya chama chake kushindwa na Zitto.
|
![]() |
|
Albert
Msando akiongea na wanahabari baada ya kushinda hukumu hiyo.
|
![]() |
|
Baadhi ya
mabango waliyokuwa nayo wananchi.
|
![]() |
|
Ulinzi mkali
nje ya Mahakama Kuu.
|
Mbunge wa Jimbo
la Kigoma Kaskazini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Bw.
Zitto Zuberi Kabwe amekigalagaza chama chake baada ya kuibuka mshindi katika
hukumu iliyosomwa na Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, John Utamwa.
Hukumu hiyo
imetolewa leo(Januari 07,2014) majira ya saa 11 jioni baada ya Zitto
kuwasilisha shauri la kuiomba mahakama iweke zuio kwa Kamati Kuu ya Chadema
(CC) kumjadili kuhusu uanachama wake.
Mahakama Kuu
imeamua Zitto aendelee kuwa mwanachama hai wa Chadema mpaka itakamalizika kesi
ya awali aliyofungua akidai Chadema kumrejeshea nyazifa zake zote alizovuliwa
na chama hicho na kwa kipindi hiki haki zote za mbunge huyo zitakuwa chini ya
uangalizi wa mahakama mpaka kesi itakapomalizika na kutolewa hukumu.
Zitto
alifungua kesi ya kudai kurejeshewa nyazifa zake ambazo alivuliwa mwishoni mwa
mwaka jana, kesi hiyo iliambatana na kesi nyingine aliyoifungua hivi karibuni
akiomba Kamati kuu isijadili kuhusu uanachama wake mpaka itakapoisha kesi yake
ya awali.
Kesi ya
awali ya mbunge huyo kudai kurejeshewa nyazifa zake itaunguruma tena Februari
13, mwaka huu.
Aidha Wakili
wa chama cha CHADEMA,Tundu Lisu ameeleza kutoridhika na maamuziki ya
Mahakama,hivyo akabanisha kuwa Zitto
Kabwe atabaki kuwa Mbunge wa Mahakama,na kama tujuavyo Mbunge wa Mahakama una muda wake basi tujipe muda tuu..alibainisha
Tundu Lisu.
















No comments:
Post a Comment