Hayo
yalisemwa na Alhaj Maalim Hassan, alipokuwa akizungunza na waandishi wa habari
ofisini kwake jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
“Natabiri
kuna kiongozi mmoja wa kisiasa mwenye nguvu katika jamii hapa nchini, atarukwa
na akili kuelekea mwisho wa mwaka huu na itakuwa anguko lake na wafuasi wake
kwenye harakati za kuimarisha ustawi wa Watanzania na dola yake,” alisema Alhaj
Hassan.
Hata hivyo,
Alhaj Hassan hakutaja jina la kiongozi huyo na sababu zitakazosababisha arukwe
na akili.
Aidha,
alitabiri kuwa mchakato wa Katiba mpya utapita kwa mbinde hususan suala la
muundo wa serikali tatu katika Muungano.
Hata hivyo,
alisema baada ya malumbano hayo, Rais Jakaya Kikwete, atatumika zaidi kuweka
mambo sawa lakini ni baada ya jamii nzima kuweweseka.
Pia, alisema
mwaka huu si mzuri kwa viongozi wa kidini kwani kuna watakaokufa ghafla na
baadhi yao wakiondolewa madarakani kwa aibu na kashfa.
Kadhalika,
utabiri unaonyesha kuwa mwaka huu hususan siku za Jumatano, kutakuwa na shida
kubwa na nyingi ikiwamo kuibuka kwa maradhi.
Kwa msingi
huo, Alhaj Hassan aliishauri serikali kuchukua tahadhari katika kukabiliana na
maradhi hayo yakiwamo malaria, kuhara damu na kichocho.
“Kwa
asilimia kubwa, utabiri uliopita wa mwaka 2013 ulikamilika kwa asilimia 90 na
mengi niliyoyatabiri mwaka jana yametokea kwani kuna mashujaa waliofariki
dunia, ajali nyingi za barabarani, angani na baharini watu kuwa na hofu na
wengine kuuawa,” alisema Alhaj Hassan.
Source:
NIPASHE






No comments:
Post a Comment