Sunderland wakiwa kwao wameifunga Manchester United Bao 2-1 katika Mechi ya Kwanza ya Nusu Fainali ya Capital One Cup. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, January 08, 2014

Sunderland wakiwa kwao wameifunga Manchester United Bao 2-1 katika Mechi ya Kwanza ya Nusu Fainali ya Capital One Cup.

Mchezaji Fabio Borini wa Sunderland akishangilia baada ya kuiangamiza Man United Jana (Januari 07,2014) usiku huku wakipata Bao lao la kwanza Kipindi cha Kwanza baada Mkongwe Ryan Giggs kujifunga.

Nemanja Vidic akishangilia baada ya kuifungia Man United bao la kusawazisha kwa kichwa la Nahodha lakini Sunderland wakapewa Penati ya utata mkubwa kufuati Adam Johnson kujiangusha Golini alipokabiliwa na Tom Cleverley na Mshika Kibendera kuashiria Penati wakati Refa Andre Marriner aliekuwa mbele ya Mpira huo hakutoa chochote wakati wa tukio..Penat hiyo ilifungwa na Borini, Mchezaji wa Mkopo kutoka Liverpool.

CAPITAL ONE CUP 2013/2014:-RATIBA/MATOKEO NUSU FAINALI.

Jumanne Januari 7,2014.

Sunderland 2 Man United 1

[Saa 4 Dakika 45 Usiku]
Jumatano Januari 8,2014.

Man City v West Ham

Marudiano
Jumanne Januari 21,2014.

West Ham v Man City

Jumatano Januari 22,2014.

Man United v Sunderland



Timu hizi zitarudiana hapo Januari 22 Uwanjani Old Trafford.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad