Tazama baadhi ya Wanyama wanaopatikana katika Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo mkoani Geita. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, January 10, 2014

Tazama baadhi ya Wanyama wanaopatikana katika Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo mkoani Geita.

Sehemu ya maji maalum ijulikanayo kama 'Maji Matakatifu' iliyopo katika Hifadhi ya kisiwa cha Rubondo ambapo samaki hupatikana kwa wingi... Pia ni sehemu ya matambiko kwa wakazi wanaoishi kuzunguka eneo la Hifadhi. Hii ni moja wapo ya sehemu ya utalii katika hifadhi hiyo.


Tembo akinywa maji ndani ya ziwa victoria katika hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo, wanyama hawa ni sehemu ya utalii katika Hifadhi hiyo.

Mnyama aina ya Sitatunga (Nzohe) ambaye anapatikana katika hifadhi ya kisiwa cha Rubondo pekee kati ya hifadhi zote 16 Tanzania,akiwa ndani ya hifadhi hiyo ya Rubondo.

Baadhi ya Mitumbwi pamoja na nyavu zinazokamatwa na askari wa hifadhi ya    Kisiwa cha Rubondo wakati wa msako wa majangili wa Samaki katika Hifadhi hiyo.


Hifadhi ya Kisiwa cha Rubondo ambayo sehemu yake kubwa iko Mkoani Geita huku sehemu ndogo ya eneo lake ikiwa katika mikoa miwili ya Mwanza na Kagera.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad