![]() |
|
Paul Kagme, rais
wa Rwanda …’’ Rwanda imeelezea mshangao wake kuona uvumi huo ukizagaa, huku
raia wa mashariki ya Congo wakiandamana wakionyesha furaha kuhusiana na na
taarifa isiyokua ya kweli…’’
|
Ikulu ya rais wa Rwanda imekanusha leo ijumaa (Januari 10,2014) uvumi kuhusu kifo cha rais
Paul Kagame, ambao umepelekea raia wa mji wa Goma kuandamana mabarabarani
wakisheherekea kwa furaha taarifa hio.
Rwanda iliingia kijeshi mara kadhaa kwenye aridhi ya Congo, hasa
ikiwaunga mkono waasi dhidi ya utawala wa Kinshasa wakati wa vita viliyoibuka
nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo ikiitwa Zaïre wakati huo, katika miaka
ya 1996-1997 na katika miaka ya 1998 hadi 2003.
Rwanda
imeelezea mshangao wake kuona uvumi huo ukizagaa, huku raia wa mashariki ya
Congo wakiandamana wakionyesha furaha kuhusiana na na taarifa isiyokua ya
kweli.
Afisa m'moja
anaefanya kazi kwenye Ikulu ya rais wa Rwanda, amefahamisha AFP kwamba taarifa
ya kifo cha rais Paul Kagame ilikua uvumi mtupu.
“ Rais
wakati huu tunaongea, anakutana kwa mazungumzo na wanafunzi wa chuo kikuu
kutoka Marekani. Muko huru kuja kuhudhuria kikao hicho, na muweze kukutana nae,
ameendelea kusema afisa huyo.
Paul Kagame,
mwenye umri wa miaka 56, ni rais wa Rwanda tangu mwaka wa 1994, baada tu ya
waasi wa RPF kushinda jeshi la Rwanda lilokua likimuunga mkono rais Juvenal
Habyarimana. Chanzo cha kushindwa kwa jeshi la Rwanda ni mauaji ya kimbari, ambayo
lilihusishwa jeshi hilo.
Watu laki
nane, wengi wao kutoka jamii ya watutsi waliuawa.
Wafuasi wa
rais Paul Kagame wanamsifu kwamba ni mtu mwenye mtazamo katika masula ya
uchumi, na lengo lake ni kuliendeleza taifa la Rwanda, huku wapinzani wake
wakimtuhumu kujihusisha na tabia mbovu ya kufuta vyama vya upinzani.
Paul Kagame
amevaa lawama, kwa mujibu wa Jumuiya ya Kimataifa, kutokana na kuunga mkono
makundi ya wapiganaji mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, licha ya
kua Kigali imeendelea kukanusha madai hayo.
Source:- Na
RFI






No comments:
Post a Comment