|
Mwanachama
wa Chadema, anayepinga hoja za Zitto Kabwe, akimtwanga mfuasi wa Zitto Kabwe.
|
Mahakama Kuu
Kanda ya Dar es Salaam, imeahirisha kutoa hukumu ya kesi iliyofunguliwa jana na
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Zuberi Kabwe (Chadema), kuhusu ombi la kuitaka
Mahakama hiyo kuizuia Kamati Kuu ya Chama hicho, kutomjadili katika kikao
ambacho kilipangwa kufanyika leo jijini Dar es Salaam.
Jaji John
Utumwa alisitisha kutoa hukumu hiyo mpaka siku ya Jumatatu (Januari 06,2014)saa
4:00 asubuhi.
Hata hiyo
baada ya Jaji huyo kuahirisha kesi hiyo, nje ya Mahakama hiyo kulikuwa na
vurugu kubwa baada ya kundi linalo unga mkono maamuzi ya Chadema kutwangana na
kundi linalo muunga Zitto Kabwe.
Hatua hiyo
ilisababisha Askari wa Jeshi la Polisi kuingilia kati, huku wakiungana na
upande wa Chadema na kuwatwanga marundi wafuasi wa Zitto waliokuwa na mambango
kama ilivyokuwa kwa wenzao wa Chadema.
Kesi hiyo
ilifunguliwa jana na wakili wa Mbunge huyo Albert Msando huku wakili wa Chadema
Tundu Lissu akiweka pingamizi,hata hivyo Jaji John Utumwa wa Mahakama hiyo
alitupilia mbali mapingamizi yote yaliyowekwa na Tundu Lissu.
Mara baada
ya kuwasili kwa Mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini, huku akiwa ameongozana watu
kadhaa wakiwamo wanasheria wake na mabaunsa, wanachama hao walianza kumzomea
huku baadhi wakimwita fisadi.
Hali hiyo
iliibua zogo katika eneo la mahakama hiyo, hali iliyowalazimu maofisa kadhaa wa
polisi kuingilia kati kwa kuamua kumchukua Zitto na kumhifadhi kwenye chumba
maalumu na kumtoa saa 6 mchana kesi yake ilipoanza kusikilizwa.
Baadhi ya
mabango ya kumkashifu yalisomeka; Zitto
tulimpenda, CCM imempenda zaidi, Zitto rudisha fedha za CCM.
Yale
yaliyomsifia yalisomeka; Zitto kama Mandela na Zitto ni Mkombozi.
Baada ya
kumalizika kusikilizwa kwa kesi hiyo, saa 12 jioni wanachama hao walianza
kurushiana ngumi, hasa baada ya kuibuliwa kwa mabango yaliyosomeka ‘Zitto
kwanza Chadema baadaye’.
Zitto
aliomba Mahakama hiyo kuzuia Kikao cha
Kamati Kuu ya Chadema kumjadili hadi
rufaa yake aliyoikata kwenye Baraza Kuu
la Chadema itakaposikilizwa na
kuamuliwa na wazuiwe kumwingilia katika utekelezaji wa majukumu yake ya ubunge
wa Kigoma Kaskazini .
Pia aliiomba
Mahakama hiyo Kuu kumwamuru Katibu Mkuu
wa Chadema, Dk Wilbroad Slaa ampatie
nakala ya mashtaka na maelezo ya uamuzi uliofikiwa na Kamati Kuu
Novemba 22, 2013 na kusababisha avuliwe nyadhifa zake ili aweze kupeleka
rufaa yake Baraza Kuu la Chadema kupinga uamuzi huo.






No comments:
Post a Comment