Simba SC imegawana pointi na KCC ya Uganda baada ya sare ya bila kufungana katika mchezo wa Kundi B, Kombe la Mapinduzi - Zanzibar. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, January 04, 2014

Simba SC imegawana pointi na KCC ya Uganda baada ya sare ya bila kufungana katika mchezo wa Kundi B, Kombe la Mapinduzi - Zanzibar.

Kipa wa KCC, Magoola Omar akiruka juu kupangua mpira kichwani kwa mshambuliaji wa Simba, Betram Mombeki ….Kwa ujumla timu zote zilitoshana nguvu na maarifa kwa dakika zote 90 za mchezo huo, huku makipa wote, Ivo Mapunda wa Simba na Magoola Omar wa KCC wakistahili sifa kwa kuokoa michomo mingi ya hatari.



Mabeki wa KCC walimdhibiti vizuri winga machachari wa Simba SC, Ramadhani Yahya Singano ‘Messi’  wakati pia beki Mkenya, Donald Mosoti Omwanwa aliiongoza vyema safu ya ulinzi ya Simba SC. 

Matokeo hayo yanazifanya Simba SC na KCC ziendelee kukabana kileleni, kila timu ikiwa na pointi nne baada ya kucheza mechi mbili.

Mapema jioni katika mchezo wa kwanza wa kundi hilo, wenyeji KMKM nao walitoshana nguvu na AFC Leopard ya Kenya kwa sare ya 0-0 pia.

Mechi za Kundi B zitahitimishwa Januari 5, kwa Simba kumenyana na KMKM na KCC na Leopard.

Michuano hiyo itaendelea leo(Januari 04,2014) kwa mechi za Kundi C, Ashanti ikimenyana na Spice Stars na Azam FC na Tusker ya Kenya Uwanja wa Amaan, wakati Uwanja wa Gombani, Pemba Clove Stars itamenyana na URA ya Uganda na Mbeya City na Chuoni.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad