Taswira Maandamano dhidi ya mauwaji ya Kanali Mamadou Ndala mashariki ya Congo aliyezikwa leo mjini Kinshasa. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, January 06, 2014

Taswira Maandamano dhidi ya mauwaji ya Kanali Mamadou Ndala mashariki ya Congo aliyezikwa leo mjini Kinshasa.


Mazishi ya Kanali Mamadou N'Dala Mustapha aliyeuawa Alhamisi juma lililopita mjini Beni Jimboni Kivu Kaskazini baada ya kushambuliwa na waasi wa Uganda ADF NALU, yatafanyika leo Jumatatu 06,2014 mjini Kinsasha. 

 Kanali huyo ambaye alipendwa sana na waakazi wa Jimbo la Kivu Kaskazini kutokana na ukakamavu wake na kuongoza jeshi la serikali kuwashinda waasi wa M23 mwaka uliopita amezikwa pamoja na askari wengine tisa wakiwemo walinzi wake wawili na wengine waliouawa jijini Kinshasa mwishoni mwa mwaka uliopita.
Wakazi wa miji ya Mashariki ya Congo wameandamana kulaani mauwaji ya kamanda aliyewamaliza wapiganaji wa M23, na kuanza kuwasaka wapiganaji wa makundi mengine ya waasi ya Kanali Mamadou Ndala, wanataka uchunguzi ufanyike kwani hawaamini ni waasi ndio walomua. 
Vikosi vya usalama wakiwazuia waandamanaji mjini Benni walokuwa wanadai uchunguzi wa kina katika mauwaji ya Kanali Mamadou Ndala.
Wanawake wakiandamana Benni kulalamiika mauwaji ya Kanali Mamadou Ndala Jan, 03 2014.
Waandamanaji katika njia kuu ya Beni kulaani mauwaji ya Kanali M. Ndala aliyewamaliza wapiganaji wa M23, na kuanza kuwasaka wapiganaji wa makundi mengine ya waasi.
Kanali Mamadou Ndala komanda wa kikosi maalum cha jeshi la  Congo linalowasaka waasi mashariki mwa nchi DRC.
Colonel Mamadou Ndala akiongozana na wanajeshi wa Kongo kuwasaka wapiganaji wa AFD Nalu.

Rais Joseph Kabila pamoja na Gavana wa Kivu Kaskazini Julien Paluku mjini Goma.
Wanajeshi wa FARDC wakiwa katika msitu wa Virunga wakisubiri katika kuwasaka wapiganaji wa AFDL Nalu.
Ndege ya Drone ya Umoja wa Mataifa huko Mashariki ya Congo.
Wanajeshi wa jeshi la taifa la Congo waelekea kutayarisha mpango wa kuwashambulia waasi wa AFDL Nalu….Picha Na:-VOA.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad