![]() |
|
Viongozi hao
wakifungua kikao hicho cha kusomwa ripoti ya ukaguzi maalum ya CAG Jana (Januari 17,2014) katika ofisi za Mkuu wa
Mkoa Kagera kutatua mgogoro uliokuwepo katika manispaa hiyo.
|
![]() |
|
Katibu
Tawala wa Mkoa wa Kagera Bw. Nassor Mnambila akifungua kikao.…hicho cha kusomwa
ripoti ya ukaguzi maalum ya CAG Jana
(Januari 17,2014) katika ofisi za Mkuu wa Mkoa Kagera.
|
![]() |
|
Mkuu wa Mkoa
wa Kagera Mh. Fabian Massawe akimkaribisha mgeni rasmi kwenye kikao hicho cha
kukamilisha Ukaguzi Maalum " Exit Meeting" cha CAG.
|
![]() |
|
Baadhi ya
waliohudhuria kikao hicho cha kusomwa ripoti ya ukaguzi maalum Jana (Januari
17,2014) katika ofisi za Mkuu wa Mkoa Kagera kutatua mgogoro uliokuwepo katika
manispaa hiyo.
|
![]() |
|
Baadhi ya
waliohudhuria kikao hicho cha kusomwa ripoti ya ukaguzi maalum Jana (Januari
17,2014) katika ofisi za Mkuu wa Mkoa Kagera kutatua mgogoro uliokuwepo katika
manispaa hiyo.
|
![]() |
|
Meya wa
Manispaa ya Bukoba, Anatory Amani (kulia) pamoja na Madiwani wa Manispaa ya
Bukoba katika kikao hicho.
|
![]() |
|
Naibu Waziri
wa TAMISEMI Mhe. Agrey Mwanri (katikati) akimsikiliza kwa makini Bw. Ludovick
Utouh.
|
![]() |
|
Taswira ya
kikao hicho katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa Jana (Januari 17,2014)
katika ofisi za Mkuu wa Mkoa Kagera kutatua mgogoro uliokuwepo katika manispaa
hiyo.
|
![]() |
|
Madiwani wa
Manispaa ya Bukoba pamoja na Mstahiki Meya Anatory Amani ambaye madiwani wa
manispaa wanamtuhumu kwa matumizi mabaya ya madaraka. (PICHA KWA HISANI YA
BUKOBA SPORTS BLOG)
|
Taarifa ya (CAG)
Utoh.
Waziri mkuu
alituomba tufanye ukaguzi maalum,
Mwaka 2013
tulifika bukoba na kufanya kikao cha kwanza na wadau.
Katika kikao
hicho nilitoa maombi ambayo mliyafuata nawashukuru,madiwani na wananchi
walitusaidia saana.
Natoa
taadhari kwamba tulikuwa na baadhi za rejea ambazo ndizo tulizofuata,tulipokea
maombi ya wananchi wengi lakini hayakuwepo katika rejea,hatukuyafanyia kazi , Kilichobainika,Tunapohitaji
maendeleo,tunafanya vitu kwa nia njema bila kufuata taratibu
Kuhusu
uwekezaji wenye mashaka kwenye kituo cha kuosha magari,zabuni haikuwa
shindanishi ni kiyume na
taratibu cha taribu anataja kifungu kilichokiukwa
Waliosaini
ni Khamis kaputa na anatory amani huku wakijua ilikuwa ni makosa kufanya hivyo
bila idhini ya kikao cha madiwani,pia kampuni husika ya ASEC ilikuwa
haijasajiliwa na BRELA. hailipi kodi TRA
2.Issue ya
Viwanja.
Kati ya
wananchi 800 waliotakiwa kugawiwa viwanja ni 300 waliogawawia kutokana na
migogoro ya viwanja kimila.
Manispaa
ilingia makubaliano na UTT kupima viwanja elfu 5 kwa kugawana faida ya asilimia
50 kwa 50 baina ya UTT manispaa ilisainiwa na kaimu meya ngalinda bila kupata
idhini ya baraza la madiwani
Pia walikopa
fedha kutoka UTT bila kupata ridhaa ya waziri mwenye thamana.
3.Issue ya
matengenzo ya barabara mpya.
Manispaa ya
bukoba iliingia mkataba na mkandarsai aitwaye KAJUNA INVESTMENT mkataba ulikuwa
wa sh 138 milioni alilipwa fedha za dharula ambazo hazikuwa na nyaraka hivyo
malipo ya mkandarasi huyu yaliongezwa hadi kufikia sh sh 227 kwa kutumia barua
iliyosainwa na tofauti na hali ya awali.haikuwapa idhini ya mkandarasi wa
serikali na kinyume na kanuni za manunuzi ya umma.anasoma kifungu kilichokiukwa
4.issue ya
Ujenzi wa soku kuu.
Utaratibu wa
kutaka kujenga soko kuu la bukoba haikupata idhini ya madiwani ya kumlipa
mkandarasi mshauri OGM milioni 789 huku pia akawaita madiwani na kuwaeleza kuwa
mkandarasi anahitaji jumla la miliini 590 milioni. Mmojawapo wa madiwani mh
lunagisa alikataa pale pale kwenye kikao.
5.Issue ya
kuhamisha wafanyabisha wa Bukoba.
Mh Meya
anatory aman aliomba mkopo kwa kazi hiyo bila kibali cha madiwani na
mawaziri.mkopo huo hata hivyo haukupatika.
6.Mkandaasi
wa OGM.
Hakuwa kwenye orodha ya walioomba zabuni ya kufanya kazi ya ukandarasi
ushauri wa kufanya kazi katika ujenzi wa soko kuu lakini alionekana kwenye
rodha baadaye ya waliolipwa .Wakandarasi wote waliolipwa fedha hizo walikuwa
hawalipi kodi TRA-hivyo TRA ina haki ya kuwadai hizo kodi.
7.Ujenzi wa
stendi kuu ya Bukoba.
Mradi huu
hakutengezwa kwenye gazeti la serikali lakini walipata mkandarasi na kumlipa
fedha za kazi hiyo kinyume na taratibu za serikali.
Gazeti lilotangaza tenda
hiyo halikupatikana.pia timu ya ukaguzi ilitembelea eneo la kazi na kubaini
kuwa mkandarasi alilipwa fedha nyingi tofauti na kazi aliyoifanya
9.Mradi wa
maji.
Kila kata
iliyopangwa kuwekwa mradi wa maji ilitakiwa kuchangia asilimia 2 hivyo kata
anakotoka meya ilitimiza kigezo na kupata huduma hiyo.
fedha za kata zilitolewa
na meya kwa kata yake.hivyo kitendo cha kata ya meya kupata huduma hakuwa na
tatizo.Tuhuma hizi kuwa meya alitoa huduma kwa kata yake ni uongo.
10.Issue ya
uuzwaji viwanja vya wazi.
Mkataba wa
kununua kiwanja kinacholalamikiwa hakufuata taratibu za ununuzi
Ni katika
bweni la sekondari ya PEACE inayomilikiwa na Meya.
Tunapendekeza kuundwa kwa
timu maalumu kuchunguza tuhuma hizi kwani katika eneo hili hatukufikia mwisho
11.Ujenzi wa
barabara:- kwa lami kwenye kata ya meya toafuti na fedha zilizoombwa.
Manispaa
iliomba milioni 30 kukarabati barabara hiyo lakini TAMISEMI ilitoa milioni 300
na walihoji TAMISEMI walisema hilo ni la kawaida hivyo tuhuma hizo ni UONGO
12.Mradi wa
Ujenzi wa Bwawa.
Hakuwahi
kujadiliwa na baraza la madiwani,ulikuwa ni mradi wa wajanja tu
13.Issue ya
wafanyabishara soko kuu kutolipa kodi.
Manispaa
Imekosa mapato sh milioni 256 zimepotea kutokana na chanzo hicho cha
wafanyabishara wa soko kuu kutolipa kodi kutokana na mgogoro unaondelea
14.Issue ya
matumizi ya gari Sm 4663.
Gari hili
limekuwa likiegeshwa kwa ofisi ya redio kasibante ya kagasheki.
Kumbukumbu za
TRA zinaonesha kuwa ni mali ya halmashauri lakini alipohojiwa Kagasheki alidai
kuwa alinunua kwa fedha zake.
Lakini halmashauri haina kumbukumbu zozote juu ya
gari hilo
Tunapendekeza
lilerejeshwe kwenye halmshauri kama ataona ni manufaa kwa wananchi lakini kama
haitawezekana basi gari hilo libadilishiwe usajili ili lionekane ni la kiraia
15.Uteuzi wa
wakala wenye upendeleo kwenye ushuru wa basi.
Zabuni ya
aliyepata rufaa ilitenguliwa kwani haikuwa imesajiliwa na mamlaka husika
Alibadilisha
jina na kuomba tena kisha kupata,muombaji aliyeomba kwa tozo ya juu alinyimwa.
Manispaa
ilifanya upendeleo na kukosa sh million 46 kwa mwaka
16:Issue ya
posho kwa madiwani katika safari ya mafunzo nje ya wilaya.
Madiwani
wawili walitakiwa kulipwa sh laki 4 kila mmoja kwa safari hawakusafiri lakini
fedha hizo hazikurudishwa kwa manispaa na kukatiwa risiti,.hazionekani zilipo
17.Issue ya
vibanda vya maduka.
Ukaguzi
hakudhibitisha kuwepo tatizo la katika dai hili kwani nyaraka zinaonesha
kutokuwepo tatizo.bali inashauri kuwepo kwa mkanganyiko na wapangaji wake
18.Issue ya
deni katika uwanja wa mpira kaitaba.
Uwanja
ulikarabatiwa na kiwanda cha sukari kagera kwa madai ya kurejeshewa fedha
zake.sehemu ya fedha hazijarudishwa.Tume inapendekeza kufanya muafaka na kiwanda
au itafute fedha za kulipa deni
19.Kutowajibika
ipasavyo kwa ukaguzi wa ndani.
Kipo kwa
ajili ya kushauri na kuziba mianya ya matumizi mabaya ya fedha.
Aliyekuwepo
amehojiwa juu ya miradi hiyo na kwamba halikuwa hajui lolote na hakuweza
kumshauri mkurugenzi ipasavyo
20.Mteuzi
katika bodi ya maji.upendeleo kwa mmoja wa madiwani.
Waziri
mwenye thamana aliteuwa
Hitimisho.
Hatukuweka
chumvi,tuliyosema ndiyo ukweli tupu.
Namshukuru
waziri mkuu kwa kunipa kazi hii ya kukaguzi katika manispaa
Utaratibu wa
uwasilisahji wa ripoti maalum tutaipeleka kwa aliyeomba ukaguzi huu.
ASANTENI
Naibu Waziri
wa TAMISEMI Mhe. Agrey Mwanri akiongea kwa niaba ya Waziri mkuu alitoa taarifa hii kama ifuatavyo
Maelekezo ya
waziri mkuu.
Makosa ya
meya Anatory kufanya makubaliano bila idhini ya madiwani na taratibu za
serikali basi ajipime mwenyewe na kujiuzuru kwa maslahi ya manispaa ya bukoba.
Akikataa
basi madiwani wamuondoe
Watumishi wa
manispaa wachukuliwe hatua
Bw Khamis
kaputa avuliwe madaraka.
Mhandisi,mweka
hazina nk wapoteze vyeo vyao
Wakandarasi
wote waliopata fedha bila taratibu wazirejeshwe.
Alipopewa
nafasi, Meya ametangaza kujiuzulu rasmi nafasi yake


















No comments:
Post a Comment