![]() |
|
Grace Simon
mwenye miaka 14 anateseka na uzito….na…ambaye mwaka huu angekuwa darasa la saba
lakini aliachishwa shule mwaka 2010 akiwa darasa la nne na walimu wakimtaka
akatibiwe.
|
Grace Simon
mwenye miaka 14 anateseka na uzito wa kupindukia wa kilo 111 (kama gunia moja la mahindi na
viroba vitatu) hali iliyomsababishia akatishwe masomo na walimu katika Shule ya
Msingi Amani, Ukonga, Ilala jijini Dar es Salaam alikokuwa anasoma.
Grace ambaye
mwaka huu angekuwa darasa la saba lakini aliachishwa shule mwaka 2010 akiwa
darasa la nne na walimu wakimtaka akatibiwe.
MAMA MZAZI
ASIMULIA.
Akizungumza
na Uwazi kuhusu mkasa mzima wa mtoto Grace, mama yake mzazi, Ashura Bakari
alisema binti yake alimzaa salama mwaka 2000 lakini ilipofikia mwaka 2002 akiwa
na miaka miwili alianza kuvimba tumbo hali ambayo hakujua chanzo chake.
ATENGWA NA
WANAFUNZI.
Mama huyo
akizungumza kwa masikitiko alisema kuwa, Grace alipofika darasa la nne, akiwa
na umri wa miaka kumi baadhi ya wanafunzi wenzake walianza kumnyanyapaa
kutokana na unene ambao ulikuwa ukiongezeka siku hadi siku.
“Walikuwa
wakimtania sana mwanangu hadi kukosa
amani. Hali hiyo iliwafanya walimu kumsimamisha masomo ili atibiwe. Hadi sasa
sijapata msaada wa kupona kwake,” alisema mama huyo huku machozi yakimtoka.
HOSPITALI
ZIMESHINDWA?
Aidha, mama
Grace aliongeza kuwa amekwishahangaika katika hospitali mbalimbali za jijini
Dar es Salaam, ikiwemo Muhimbili bila mafanikio.
“Muhimbili
waliniambia ili mwanangu aweze kufanyiwa vipimo pamoja na matibabu gharama zake
ni shilingi laki nane (800,000) ambazo nimezikosa na hakuna mtu wa kunisaidia,”
alisema.
NDUGU NAO.
Alisema
mbali na kutafuta tiba hospitalini, amekuwa akipita huku na huko kuomba msaada
wa fedha kutoka kwa ndugu na jamaa lakini hakuna aliyemsadia.
KWA NINI
BABA MZAZI ASIMSAIDIE?
Katika hali
ya kushangaza, mama huyo alisema ili kupata fedha hizo anahangaika peke yake
kwa sababu baba mzazi wa Grace, Simon alikataa kutoa msaada wowote.
“Baba yake
yupo hai, alikuwa anatoa msaada kipindi cha mwanzo lakini miaka kama mitano
imepita hakuna msaada anaonipa. Ni kweli hatuishi pamoja lakini mtoto tulizaa
wote,” alisema kwa masikitiko makubwa mama huyo.
WALICHOKIONA
MADAKTARI.
Akizungumzia
kiini cha tatizo, mama huyo alisema: “Kwa mujibu wa madaktari mwanangu
anasumbuliwa na moyo kujaa mafuta mengi, kwa hiyo homoni zake zimekosa uwiano
na ini pia lina sumu nyingi.”
GRACE AWALILIA WATANZANIA.
Akizungumza
na mwandishi wetu, mtoto huyo anayetamani kuendelea kusoma aliwaomba Watanzania
wamsaidie fedha ili aweze kutibiwa na kurejea darasani.
“Niliachishwa
shule ili nitibiwe, nikipona nirejee shuleni, lakini hadi sasa sijapata nafuu,
na ninajua ni kutokana na kutopata matibabu sahihi,” alisema Grace huku akilia.
UONGOZI WA
SHULE.
Mmoja wa walimu
waandamizi wa Shule ya Msingi Amani alipokuwa akisoma mwanafunzi huyo
(hakuwa tayari kutaja jina lake),
alikiri kumtambua mwanafunzi huyo na kusema aliachishwa shule kwa hofu ya uongozi wa shule.
“Hatukumwachisha
shule kwa nia mbaya, lakini lengo letu lilikuwa akatibiwe kisha arudi shuleni
lakini matibabu anayopata hajaweza kupona na hali aliyokuwa nayo inazidi
kuongezeka siku hadi siku,” alisema mwalimu huyo.
Akaongeza:
“Mwaka huu Grace ilikuwa awe darasa la saba, lakini hata kutembea ni tatizo
hali ambayo tuliona kuwa unene ule si afya bali ni ugonjwa.”
MSAADA
UNAAOHITAJIKA.
Kwa yeyote
aliyeguswa na tatizo la Grace ambaye anasaka shilingi laki nane tu ili atibiwe,
anaweza kuwasiliana na mama yake mzazi
kwa simu: 0719 465445, ASHURA BAKARI.








No comments:
Post a Comment