![]() |
|
Waziri Mkuu
wa zamani wa Israel, Ariel Sharon enzi za uhai wake….Alikuwa katika hali ya
umahututi kwa miaka nane tangu mwaka 2006.
|
Waziri Mkuu
wa zamani wa Israel, Ariel Sharon amefariki dunia leo Januari 11, 2014 akiwa na umri wa miaka 85.
Sharon,
aliyekuwa Waziri Mkuu wa 11 wa taifa hilo la kiyahudi, alikuwa kiongozi wa
chama cha Likud, lakini katika mzozo mkubwa ndani ya chama hicho kufuatia
tofauti za kimtizamo kuhusu ukanda wa Gaza, alijitoa Novemba 2005 na kuanzisha
chama chake cha Kadima akiwa bado madarakani.
Alitegemewa
kushinda katika uchaguzi uliotarajiwa kufanyika baadaye, lakini ghafla Januari
4 mwaka 2006 alipata ugonjwa wa kupooza mwili mzima na alibakia katika hali
hiyo mbaya kwa muda wa miaka nane hadi alipofariki leo Januari 11, 2014.






No comments:
Post a Comment