Mwili wa wa aliyekuwa Waziri wa Fedha Marehemu Dkt. Willium Mgimwa Wawasili Kutoka Nchini Afrika Kusini. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, January 04, 2014

Mwili wa wa aliyekuwa Waziri wa Fedha Marehemu Dkt. Willium Mgimwa Wawasili Kutoka Nchini Afrika Kusini.


Ndege iliyoubeba mwili wa aliyekuwa Waziri wa Fedha Marehemu Dkt. Willium Mgimwa Ilipowasili katika uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere Leo (Januari 04,2014) Kutokea Nchini Afrika Kusini alipokutwa na Mauti siku chache zilizopita.



Mjane Mama Jane Mgimwa(katikati) akiwa na Balozi wa Tanzania nchini Afrika kusini Radhia Msuya(kulia) mara baada ya kuwasili kutoka nchini Afrika kusini


Naibu Waziri Wizara ya Fedha Saada Mkuya(kulia) akimsindikiza Mke wa Marehemu Mama Jane Mgimwa(katikati)katika chumba cha mapumziko mara baada ya kuwasili katika katika uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere Leo(Januari 04,2014).Kushoto ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Mh. Sophia Simba.


Baadhi ya Viongozi wa Serikali na Wabunge waliojitokeza kuupokea mwili wa aliyekuwa Waziri wa Fedha Dkt. Willium Mgimwa.


Katibu Mkuu Kiongozi Ombeni Sefue akitoa heshima kwa kugusa Jeneza Lililobeba mwili wa aliyekuwa Waziri wa Fedha Marehemu  Dkt. Willium Mgimwa Katikati ni Waziri wa Ujenzi Mh. John Magufuli na wa Mwisho ni Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Mh.Fenella Mukangara.


Mwili wa aliyekuwa Waziri wa Fedha Marehemu Dkt. Willium Mgimwa Ukiingizwa kwenye gari Maalum Tayari kwa ajili ya kuelekea nyumbani kwa marehemu kwa taratibu nyingine za mazishi.


Mkurugenzi wa Idara ya Habari(MAELEZO) Bw. Assah Mwambene (wa kwanza Kushoto)akisalimiana na baadhi wa Watu waliofika kuupokea Mwili wa wa aliyekuwa Waziri wa Fedha Marehemu Dkt. Willium Mgimwa Leo(Januari 04,2013) Jijini Dar es Salaam… Picha na Hassan Silayo-MAELEZO.


Ratiba ya mazishi ya marehemu Waziri, Dk William Mgimwa (Mb).


TAREHE 4/ 01/ 2013

  • MWILI WA MAREHEMU UNATARAJIA KUWASILI UWANJA WA NDEGE WA JULIUS NYERERE TERMINAL II, SAA7: 00 MCHANA. BAADA YA KUWASILI UTAPELEKWA NYUMBANI KWA MAREHEMU MIKOCHENI B.

  • SAA 11:00 JIONI MWILI UTAPELEKWA HOSPITALI YA LUGALO.

TAREHE 5/ 01/ 2013

  • SAA 3:00 HADI SAA 4:00 ASUBUHI:- CHAKULA NYUMBANI KWA MAREHEMU.

  • SAA 4:30 ASUBUHI :- MWILI KUWASILI NYUMBANI MIKOCHENI B.

  • SAA 5:30 HADI SAA 8:00 MWILI UTAPELEKWA UKUMBI WA KARIMJEE KWA AJILI YA SHUGHULI ZA IBADA NA HESHIMA ZA MWISHO.

  • SAA 8:10 MWILI UTAPELEKWA UWANJA WA NDEGE WA MWALIMU NYERERE TERMINAL I.

  • SAA 10:00 MWILI UNATARAJIA KUWASILI IRINGA UWANJA WA NDULI  NA KUAGWA KATIKA UKUMBI WA SIASA NI KILIMO-IRINGA

  • SAA 11:30 JIONI MWILI UTASAFIRISHWA KUELEKEA KIJIJI  CHA MAGUNGA.

TAREHE 6/ 01/ 2013 
SAA 6:00 MCHANA SHUGHULI ZA MAZISHI KIJIJINI KWA MAREHEMU MAGUNGA.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad