MATOKEO EPL 2013/2014:- Arsenal yapunguzwa kasi ,Liverpool yaiburuza Everton huku Juan Mata kiiongoza Manchester United kuiadhibu Cardiff City. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, January 29, 2014

MATOKEO EPL 2013/2014:- Arsenal yapunguzwa kasi ,Liverpool yaiburuza Everton huku Juan Mata kiiongoza Manchester United kuiadhibu Cardiff City.


MBALI na kipigo cha mabao 4-0 kutoka Liverpool usiku huu, Everton ilipata pigo lingine baada ya mshambuliaji wake tegemeo, Romelu Lukaku kutolewa nje kwenye machela katika mechi hiyo ya mahasimu wa Merseyside baada ya kuumia.


Mshambuliaji huyo wa mkopo kutoka Chelsea, aliumia kifundo cha mguu baada ya kuangukiwa na mchezaji mwenzake Gareth Barry akijaribu kumzuia bila mafanikio Steven Gerrard kufunga bao la kwanza.

Nafasi ya Lukaku ilichukuliwa na Steven Naismith dakika ya 25 tu ya mchezo huo Uwanja wa Anfield.

Mshambuliaji huyo wa Ubelgiji akitolewa nje kwa machela baada ya kuumia na kushindwa kuendelea na mchezo, Romelu Lukaku aliumia  baada ya kuangukiwa na Gareth Barry


Nyota wa Southampton, Adam Lallana, katikati, akishangilia baada ya kuifungia timu yake bao la kusawazisha dhidi ya Arsenal ambapo bao la Adam Lallana limeosha kuipa sare ya 2-2 Southampton katika mchezo wa Ligi Kuu ya England dhidi ya vinara, Arsenal ambao sasa wanawafungulia milango Manchester City na Chelsea kwenye mbio za ubingwa. 

Nyota huyo wa kimataifa wa England alifunga kiasi cha dakika mbili baada ya Santi Cazorla kuifungia Arsenal dakika ya 52 na kumuachia presha kocha Arsene Wenger katika kampeni za ubingwa. 

Southampton ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia kwa Jose Fonte dakika ya 21, lakini Oliver Giroud akaisawazishia The Gunners dakika ya 48. Arsenal walimaliza mechi wakiwa 10 baada ya Mathieu Flamini kuonyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja. 

Arsenal sasa inakuwa na pointi 52 baada ya kucheza mechi 23, ikifuatiwa na Manchester City yenye pointi 50 na Chelsea pointi 49, ingawa zote zimecheza mechi 22.


Kiungo wa Arsenal, Santi Cazorla, katikati, akishangilia na wenzake baada ya kufunga bao la pili na kutoka  sare ya 2-2 na Southampton katika mchezo wa Ligi Kuu ya England dhidi ya vinara, Arsenal ambao sasa wanawafungulia milango Manchester City na Chelsea kwenye mbio za ubingwa.



Mchezaji ghali kwenye historia ya klabu ya Man Utd Juan Mata alivaa jezi yake namba 8 ya Man United baada ya kutengeneza bao la kwanza la timu hiyo lililofungwa na Robin van Persie katika ushindi wa 2-0 dhidi ya cardiff City Uwanja wa Old Trafford jana (Januari 28,2014) usiku huu.


Robin van Persie akipongezwa na wenzake baada ya kufunga bao la kwanza akirejea kutoka kwenye majeruhi Katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya England, ilibidi kocha David Moyes asuburi hadi dakika ya 59 kujihakikishia ushindi kwa bao zuri la shley Young.

Matokeo hayo yanaifanya United itimize pointi 40 baada ya kucheza mechi 23, ikibaki nafasi ya saba.

 RATIBA YA MECHI ZA LEO EPL 2013 / 2014   JANUARI 29,2014.
 



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad