![]() |
|
Sehemu ya juu ya jengo la benki ya PJ Morgan
(iliyozungushiwa mduara mwekundu) ambayo mtu huyo anasemekana alijirusha na
kuangukia sehemu ya chini (yenye mduara) na kufa.
|
Mtu mmoja
mwenye umri wa miaka 39, amefariki leo(Januari 28,2014) asubuhi majira ya saa mbili baada ya
kuanguka kutoka jengo la makao makuu ya benki ya JP Morgan mjini London,
Uingereza, eneo la Canary Wharf.
Inasemekana
mtu huyo alijirusha kutoka sehemu ya juu ya jengo hilo na kuanguka katika
sehemu ya juu iliyotokeza mbele ya jengo hilohilo kabla ya kufika chini.
Polisi
walisema walimkuta mtu huyo katika ghorofa ya tisa ambapo wanayafahamu maelezo
yake lakini wanasubiri utambulisho zaidi, na kwamba hakuna aliyekamatwa
kuhusiana na tukio hilo hadi sasa na kwamba uchunguzi unaendelea.







No comments:
Post a Comment