Football Results 2013/2014:-Manchester City wazidi kuwa mshindani mkuu wa Arsenal kileleni, Real Madrid na ushindi bao 5-0 kwenye Mechi ya La Liga huku Vinara wa Serie A, Juventus wakibaki kileleni wakiwa Pointi 8 mbele ya AS Roma. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, January 19, 2014

Football Results 2013/2014:-Manchester City wazidi kuwa mshindani mkuu wa Arsenal kileleni, Real Madrid na ushindi bao 5-0 kwenye Mechi ya La Liga huku Vinara wa Serie A, Juventus wakibaki kileleni wakiwa Pointi 8 mbele ya AS Roma.

Mchezaji Santi Cazorla akishangilia baada ya kuifungia Arsenal na kuifanya Arsenal ijiimarisha zaidi  kileleni mwa Ligi Kuu ya Uingereza kufuatia ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Fulham jana jioni(Januari 18,2014) wakiwa  Uwanja wa Emirates…kwa mchezaji wao  Santi Cazorla kufunga mabao hayo katika dakika ya 57 akimalizia pasi ya Jack Wilshere na la pili dakika ya 62. Arsenal sasa inatimiza pointi 51 baada ya kucheza mechi 22.

Arsenal wanabakia nafasi ya kwanza kileleni mwa msimamo wa Ligi  wakiwa Pointi 1 mbele ya Man City na Pointi 5 mbele ya Timu ya 3 Chelsea ambao Jumapili (Januari 19,2014) wako kwao Stamford Bridge kuivaa Man United.
Mchezaji Edin Dzeko akishangilia baada ya kuifungia bao la 100 kwa Manchester City dhidi ya Cardiff na kuifanya Timu ya Manchester City ifunge goli la 100 katika mashindano yote msimu huu, na Nyota huyo wa Bosnian hilo linakuwa bao lake la 16 msimu huu, wakati Negredo amefunga 21 na Aguero 20, hao wakiwa wafungaji bora wa City.

Man City, wakicheza kwao Etihad, waliichapa Cardiff City Bao 4-2 na kuzidisha presha kwa Vinara Arsenal kwa wao kubakia Nafasi ya Pili Pointi 1 nyuma yao.

Bao za Man City zilifungwa na Dzeko, Navas, Toure na Aguero huku za Cardiff zikifungwa na Noone na Campbell.

MAN CITY ILIVYOTIMIZA MABAO 100 MSIMU HUU

BAO   TAREHE   DAKIKA  MFUNGAJI   WAPINZANI
La 1      19/08/2013    6          Silva               Newcastle United    Nyumbani      
La 10    17/09/2013    53        Yaya Toure    Viktoria Plzen          Ugenini      
La 25    05/10/2013    45        Aguero          Everton                     Nyumbani      
La 50    24/11/2013    50        Aguero          Tottenham Hotspur  Nyumbanj    
La 75    17/12/2013    53        Dzeko            Leicester City          Ugenini     
LIVERPOOL imetoka nyuma kwa mabao 2-0 na kulazimisha sare ya 2-2 na Aston Villa Jana(Januri 18,2014) Uwanja wa Anfield katika mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza ambapo Aston Villa walitangulia kupata mabao yao kipindi cha kwanza kuptia kwa Weimann dakika ya 26 na Benteke dakika ya 36,  Sturridge akaifungia Liverpool la kwanza dakika ya 45 kabla ya Gerrard kufunga la pili kwa penalti dakika ya 53, baada ya Suarez kuangushwa. Hata hivyo, penalti hiyo ililalamikiwa na Villa,wakimtuhumu Suarez kujiangusha.

Matokeo hayo yanaifanya Liverpool ifikishe pointi 43 baada ya kucheza mechi 22 na inabaki nafasi ya tatu nyuma ya Chelsea yenye pointi 46, Man City 50 na Arsenal 51.


Katika mechi nyingine za ligi hiyo Jana (Januari 18,2014), Sunderland ilitoka sare ya 2-2 na Southampton, Crystal Palace imeifunga 1-0 Stoke City, Norwich City imeifunga 1-0 Hull City na West Ham United imelala 2-1 nyumbani mbele ya Newcastle United.

League Table 2013/2014 EPL.


Position Team Played Goal Difference Points
1 Arsenal 22 24 51
2 Man City 22 38 50
3 Chelsea 21 21 46
4 Liverpool 22 25 43
5 Everton 21 15 41
6 Tottenham 21 1 40
7 Man Utd 21 11 37
8 Newcastle 22 4 36
9 Southampton 22 4 31
10 Aston Villa 22 -7 24
11 Hull 22 -6 23
12 Norwich 22 -17 23
13 Stoke 22 -14 22
14 Swansea 21 -4 21
15 West Brom 21 -5 21
16 Crystal Palace 22 -17 20
17 Fulham 22 -26 19
18 West Ham 22 -11 18
19 Sunderland 22 -15 18
20 Cardiff 22 -21 18
Wakiwa Ugenini huko Estadio Benito Villamarín, Real Madrid wakiongozwa na Mchezaji Bora Duniani, Cristiano Ronaldo, Jana (Januari 18,2014) wakaitandika Real Betis Bao 5-0 kwenye Mechi ya La Liga.

Bao za Real zilifungwa na Cristiano Ronaldo, Gareth Bale, Karim Benzema, Angel Di Maria na Alvaro Morata.
Ushindi huu umeifanya Real ifungane kwa Pointi na Vinara Barcelona na Atletico Madrid, zote zikiwa na Pointi 50 kila mmoja, huku Barca wakiongoza wakifuatia Real na Atletico ipo Nafasi ya 3.

Lakini Barca na Atletico zina Mechi moja mkononi ambazo watacheza Jumapili (Januari 19,2014).

14:00 Getafe CF v Real Sociedad

19:00 Villarreal CF v UD Almeria

21:00 Levante v FC Barcelona

23:00 Atletico de Madrid v Sevilla FC

League Table 2013/2014 La Liga.


Position Team Played Goal Difference Points
1 Barcelona 19 41 50
2 Real Madrid 20 37 50
3 Atlético Madrid 19 36 50
4 Athletic Bilbao 19 8 36
5 Villarreal 19 16 34
6 Real Sociedad 19 8 32
7 Sevilla 19 6 30
8 Espanyol 20 -2 25
9 Valencia CF 20 -5 24
10 Granada CF 20 -6 24
11 Levante 19 -9 23
12 Getafe 19 -11 23
13 Osasuna 20 -12 22
14 Málaga 20 -5 21
15 Elche 20 -9 21
16 Celta de Vigo 20 -9 19
17 Almería 19 -17 19
18 Real Valladolid 19 -12 16
19 Rayo Vallecano 20 -28 16
20 Real Betis 20 -27 11


Mabingwa na Vinara wa Serie A, Juventus, Jana (Janauari 18,2014) waliicharaza Sampdoria Bao 4-2 na kuendelea kubaki kileleni wakiwa Pointi 8 mbele ya AS Roma ambayo Jana pia waliitwanga Livorno Bao 3-0.
Katika Mechi ya Juve iliyochezwa Juventus Stadium, Bao za Mabingwa hao zilifungwa na Arturo Vidal, Bao 2 moja Penati, Fernando Llorente na Paul Pogba huku Bao za Sampdoria zikipachikwa na Andrea Barzagli, aliejifunga mwenyewe, na Manolo Gabbiadini.

Kwenye Mechi ya AS Roma na Livorno Bao za Roma zilifungwa na Mattia Destro, Kevin Strootman na Adem Lajajic.

League Table 2013/2014 Serie A


Position Team Played Goal Difference Points
1 Juventus 20 36 55
2 Roma 20 32 47
3 Napoli 19 21 42
4 Fiorentina 19 14 37
5 Internazionale 19 15 32
6 Verona 19 4 32
7 Torino 19 4 26
8 Parma 19 3 26
9 Lazio 19 -3 24
10 Genoa 19 -5 23
11 Milan 19 1 22
12 Atalanta 19 -9 21
13 Cagliari 19 -9 21
14 Sampdoria 20 -7 21
15 Udinese 19 -10 20
16 Chievo 19 -10 17
17 Sassuolo 19 -20 17
18 Bologna 19 -16 16
19 Catania 19 -21 13
20 Livorno 20 -20 13

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad