Katibu Mkuu
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Wilbrod Slaa amesema
hawaogopi kuita Baraza Kuu la chama hicho ili kusikiliza rufaa ya aliyekuwa
Naibu Katibu Mkuu Zitto Kabwe kama inavyodaiwa na baadhi ya watu.
Alisema
chama hicho kitaitisha kikao hicho hivi karibuni ili kusikiliza utetezi wa
Kabwe ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini kupitia Chadema.
Akihutubia
mamia ya wakazi wa manispaa ya Iringa na vitongoji vyake katika uwanja wa
Mbwetogwa juzi , Dk Slaa alisema Zitto alivuliwa nafasi zake za uongozi ndani
ya chama hicho baada ya kubainika amekiuka maadili ya chama.
“Hata nikiwa
mimi aua Mwenyekiti wangu Freman Mbowe au kiongozi mwingine yoyote yule au
mwanachama, akikiuka maadili ya chama ni lazima achukuliwe hatua za kinidhamu,”
alisema.
Alisema
hivisasa Zitto aruhusiwi kufanya shughuli za kichama kupitia jukwaa la Chadema
kwa kuwa si kiongozi tena wa Chadema, rufaa yake haijasikilizwa na kafungua
kesi mahakamani.
“Wanachama,
wapenzi na wadau wote wa Chadema msimpe ushirikiano wowote Zitto mpaka sula
lake litakapohitimishwa,” alisema.
Alisema
oparesheni ya M4C Pamoja Daima haifanywi na chama hicho kwa ajili ya
kusmshughulikia Kabwe, inafanywa ikiwa ni maandalizi yao ya kuelekea uchaguzi
wa serikali za mitaa utakaofanyika baadaye mwaka huu.
Akinukuliwa
na gazeti la jamboleo la jana, Kabwe amesema hakuna wa kumzuia kufanya mikutano
nchini.
Kwa kupitia
taarifa ya gazeti hilo alinukuliwa akisema “kama kuna mtu anadhani sitaweza
kufanya mkutano wa aina yoyote katika maeneo mbalimbali nchini anajidanganya,
nitazunguka kuzungumza na wananchi kwa maslahi ya taifa hili na ni haki yangu
kikatiba.”
Alisema
atafanya mikutano hiyo kama mbunge kwa kuwa ni wajibu wake kikatiba kuzungumza
na wananchi kuhsusu mambo mbalimbali.
Wengine
waliohutubia mkutano huo ni pamoja na Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini,
Mchungaji Peter Msigwa na Mbunge wa Kawe Dar es Salaam, Halima Mdee.
Viongozi hao
walitumia fursa waliyopewa kujibu hoja mbalimbali zinazotolewa na viongozi wa
Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani Iringa zikimponda mbunge wa jimbo la Iringa
Mjini anayedaiwa kashindwa kutekeleza ahadi zake alizotoa wakati wa Uchaguzi
Mkuu wa 2010.
Katika
mkutano huo, Dk Slaa pia aliwapokea na kuwapa kadi za Chadema, wanachama wanne
kutoka CCM, TLP na NCCR- Mageuzi.





No comments:
Post a Comment