Timu ya Coastal Union U 20 imkefanikiwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Uhai kwa kuichapa Yanga kwa mabao 2-0. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, December 01, 2013

Timu ya Coastal Union U 20 imkefanikiwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Uhai kwa kuichapa Yanga kwa mabao 2-0.


Coastal Union (U 20) ambayo iliingia fainali baada ya kuivua ubingwa Azam Fc ilionyesha soka safi na la kuvutia. Na Juma Mahadh na Ally Ufud wakafanya kweli kwa kufunga mabao hayo mawili.

Baada ya kupata bao la kwanza, Coastal ilizidi kuwa bora na kuipa Yanga wakati mgumu zaidi.

Bao la pili lilipatikana katika dakika ya 88 huku Yanga wakiamini walikuwa wanakaribia kusawazisha.

Nao  Azam FC imefanikiwa kushika nafasi ya tatu katika michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 20 kwa klabu za Ligi Kuu ya Bara, maarufu kama Kombe la Uhai, baada ya kuifunga kwa penalti 3-1 Mtibwa Sugar kufuatia sare ya 3-3 ndani ya dakika 120 Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

Dakika 90 za mchezo huo zilimalizika timu hizo zikiwa zimefungana mabao 2-2 na zilipoongezwa dakika 30 kila timu ikapata bao moja zaidi.

Mabao ya Azam yalifungwa na Eric Haule dakika ya 32, Adam Omary dakika ya 38 na Ahmed Abbas dakika ya 109, wakati mabao ya Mtibwa yalifungwa na Ally Makarani dakika ya 16, Hassan Mbande dakika ya 81 na Issa Kiganga kwa penalty dakika ya 105.

Penalti za Azam zilifungwa na Mgaya Abdul, Shiraz Abdallah na Ahmed Abbas, wakati ya Mtibwa ilifungwa na Jumanne Mlindwa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad