Mabingwa wa Uingereza Manchester United huko ugenini katika dimba la White Hart Lane walazimisha kutoka Sare ya Bao 2-2 na Tottenham. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, December 01, 2013

Mabingwa wa Uingereza Manchester United huko ugenini katika dimba la White Hart Lane walazimisha kutoka Sare ya Bao 2-2 na Tottenham.

Mshambuliaji wa Manchester United, Wayne Rooney akiisawazishia timu yake kwa penalti dhidi ya Spurs na kuwa amefunga magoli  mawili leo (Desemba 01,2013) na kuinusuru Manchester United kulala mbele ya kikosi cha Andre Villas-Boas, Tottenham baada ya kupata sare ya 2-2 Uwanja wa White Hart Lane katika mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza(EPL).

Rooney akisngilia baada ya kuifungia United  alisawazisha dakika ya 32 baada ya krosi ya Phil Jones kushindwa kudhibitiwa na Walker na kutua kwa Rooney aliekwamisha wavuni.
Sandro akishangilia baada ya kuifungia Tottenham akiifumua mzinga wa Mita 25 na kuipa Spurs Bao la Pili dakika ya 54 .


Mabingwa wa Uingereza, Manchester United, leo (Desemba 01,2013) wakicheza Mechi ya Ligi Kuu EPL huko ugenini katika dimba la  White Hart Lane ,walilazimika kutoka nyuma mara mbili na kusawazisha na kutoka Sare ya Bao 2-2 na Tottenham.

Tottenham, ambao ndio kwanza wametoka kwenye kipondo cha Bao 6-0 walichoshushiwa na Man City Wiki iliyopita, leo walitangulia kufunga kwa Bao la awali la frikiki ya Kyle Walker  dakika ya 18 akini Wayne Rooney alisawazisha dakika ya 32 baada ya krosi ya Phil Jones kushindwa kudhibitiwa na Walker na kutua kwa Rooney aliekwamisha wavuni.

Kipindi cha Pili, Sandro alifumua mzinga wa Mita 25 na kuipa Spurs Bao la Pili dakika ya 54 lakini Dakika 3 baadae Rooney katika dakika ya 57 aliisawazishia Man United kwa Penati baada Kipa Hugo Lloris kumchezea Danny Welback.

LIGI KUU ENGLAND RATIBA.

[Saa za Bongo]

Jumanne Desemba 3,2013.

20:00 Crystal Palace v West Ham

Jumatano Desemba 4,2013.

22:45 Arsenal v Hull
22:45 Liverpool v Norwich
22:45 Man United v Everton
22:45 Southampton v Aston Villa
22:45 Stoke v Cardiff
22:45 Sunderland v Chelsea
22:45 Swansea v Newcastle
23:00 Fulham v Tottenham
23:00 West Brom v Man City
 
MSIMAMO:-2013/2014.

NA
TIMU
P
GD
PTS
1
Arsenal
13
17
31
2
Liverpool
12
11
24
3
Chelsea
12
11
24
4
Everton
13
8
24
5
Newcastle
13
1
23
6
Man City
12
22
22
7
Southampton
12
8
22
8
Man United
13
5
22
9
Tottenham
13
-3
21
10
Aston Villa
13
-1
16
11
Swansea
12
1
15
12
West Brom
13
-1
15
13
Hull
12
-6
14
14
Norwich
13
-12
14
15
West Ham
13
-2
13
16
Stoke
13
-6
13
17
Cardiff
13
-9
13
18
Fulham
13
-13
10
19
Sunderland
13
-16
8
20
Crystal Palace
13
-15
7

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad