Viongozi wa
Jumia ya Afrika Mashariki EAC, wametia saini makubaliano ya kuanzisha mfumo wa
pamoja wa fedha utakaopelekea nchi tano wanachama kuwa na sarafu moja.
Marais
Yoweri Museveni wa Uganda, Uhuru Kenyatta wa Kenya Jakaya Kikwete wa Tanzania,
Paul Kagame wa Rwanda na Pierre Nkurunziza wa Burundi walifikia makubaliano
hayo wakati wa mkutano wao siku ya Jumamosi(Novemba 30,2013) mjini Kampala.
Kabla ya
kutia saini mkataba huo Rais Kenyatta amesema "huu ni wakati wa kihitoria
na muhimu kwa jumiya yetu". Mkataba huo unaanzisha awamu ya mwisho ya
mataifa hayo matano kuanza kuondowa sarafu zao na kuanzisha sarafu moja ya
Afrika Mashariki.
Wakati wa
mkutano huo viongozi hao walitia pia sahihi mkataba wa kuanzisha Baraza la
Amani na Usalama la EAC, litakaloshughulikia vitisho vya usalama katika kanda
hiyo. Tayari EAC inajivunia Umoja wa Forodha na Soko la Pamoja kwa wakazi
milioni 135.
Na wakati wa mkutano huo wa 15 wa viongozi
Uganda iliikabidhi Kenya uwenyekiti jumiya hiyo unaozunguka kwa zamu.











No comments:
Post a Comment