LIGI KUU ENGLAND RATIBA/MATOKEO.
Jumamosi Novemba 30,2013.
Cardiff 0 Arsenal 3
Everton 4 Stoke 0
Norwich 1 Crystal Palace 0
West Ham 3 Fulham 0
EVERTON 4 - 0 STOKE
Bao za Deulofeu, Coleman, Oviedo na Lukaku, leo zimewapeleka Everton juu na kukamata Nafasi ya 4 katika Msimamo wa Ligi Kuu England walipoibwaga Stoke City Bao 4-0 Uwanjani Goodison Park.
WEST HAM 3 -0 FULHAM
Sasa, bila shaka, Meneja wa Fulham, Martin Jol, yuko hatarini kumwaga unga baada ya Timu yake kuchapwa Bao 3-0 na West Ham walipocheza Ugenini Uwanja wa Upton Park.
Bao za West Ham zilifungwa na Diame, Carlton Cole na Joe Cole.
CARDIFF CITY 0 - 3 ARSENAL
Bao 2 za Aaron Ramsey na moja la Mathieu Flamini zimewapa Arsenal ushindi wa Bao 3-0 walipocheza Ugenini na Cardiff City.
Ushindi huu umewafanya Arsenal wazidi kupaa kileleni wakiwa Pointi 7 mbele.
NORWICH 1 - 0 CRYSTAL
Bao la Dakika ya 30 la Gary Hooper, limewapa Norwich City ushindi wa Bao 1-0 walipocheza na Crystal Palace waliokuwa na Menja mpya Tony Pulis ambae leo ndio rasmi alikuwa akianza kazi.
Kipigo hichi kimewabakisha Palace mkiani na Norwich kupanda hadi Nafasi ya 14.
LIGI KUU ENGLAND RATIBA.
[Saa za Bongo]
Jumapili Desemba 1,2013.
15:00 Tottenham v Man United
17:05 Hull v Liverpool
19:10 Chelsea v Southampton
19:10 Man City v Swansea





No comments:
Post a Comment