Kilimanjaro Stars na ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya Somalia katika mchezo wa Kundi B, Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, December 01, 2013

Kilimanjaro Stars na ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya Somalia katika mchezo wa Kundi B, Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge.


Kwa matokeo hayo,Kilimanjaro  Stars imetimiza pointi nne baada ya awali kutoa sare ya 1-1 na Zambia katika mchezo wake wa kwanza na mustakabali wake wa kuingia Robo Fainali utategemea matokeo ya mechi za mwisho za kundi hilo.


Beki wa Somalia, Aden Hussein Ibrahim akimpitia mfungaji wa bao pekee la Stars, Haroun Chanongo Uwanja wa Nyayo leo(Desemba 01,2013). 
Picha Juu:- Ramadhani Singano kulia na Frank Domayo kushoto wakimpongeza Chanongo katikati kwa kufunga bao hilo.
Bao pekee la Haroun Athumani Chanongo dakika ya 57 limetosha kuipa Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya Somalia mchana wa leo(Desemba 01,2013)  katika mchezo wa Kundi B, Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge Uwanja wa Nyayo, Nairobi, Kenya. 

Kwa matokeo hayo, Stars imetimiza pointi nne baada ya awali kutoa sare ya 1-1 na Zambia katika mchezo wake wa kwanza na mustakabali wake wa kuingia Robo Fainali utategemea matokeo ya mechi za mwisho za kundi hilo.


Katika mchezo wa leo, Stars ilikuwa inaanza vizuri kutokea nyuma, lakini wanapofika kwenye eneo la wapinzani wanaharibu, ama kwa kupeana pasi mbovu au kupokonywa mipira kirahisi.

Na hakukuwa na uelewano kabisa baina ya washambuliaji wa Stars, Elias Maguri, Amri Kiemba na Mrisho Ngassa hali ambayo ilifanya mabeki wa Somalia wacheze kwa uhuru zaidi.

Somalia walicheza vizuri kipindi cha kwanza na kukosa mabao mawili ya wazi, kutokana na juhudi za kipa Ivo Mapunda kuokoa hatari zote.

Kipindi cha pili, kocha Mdenmark Kim Poulsen alianza na mabadiliko, akiwatoa Kiemba na Maguri na kuwaingiza washambuliaji wawili a Simba SC, Ramadhani Singano na Haroun Chanongo ambao walibadilisha mchezo.

Pasi nzuri ya Singano ‘Messi’ iliunganishwa nyavuni na Chanongo dakika ya 57 kuipatia Stars bao hilo pekee.

Baada ya bao hilo, Stars iliendelea kushambulia kupitia kwa Singano na Chanongo, lakini wakaishia kukosa mabao ya wazi. Somalia nayo iliendelea kushambulia lango la Stars na kuishia kukosa mabao mawili ya wazi, sifa zimuendee Ivo Mapunda.

Kim Poulsen alimtoa Mrisho Ngassa dakika ya 79 na kumuingiza Farid Mussa, lakini mabadiliko hayo hayakuleta jipya upande wa Stars.

Kikosi cha Stars leo kilikuwa; Ivo Mapunda, Himid Mao, Erasto Nyoni, Said Morad, Kevin Yondan, Frank Domayo, Salum Abubakar, Athumani Iddi ‘Chuji’, Elias Maguri/Haroun Chanongo dk46, Amri Kiemba/Ramadhani Singano ‘Messi’ dk46 na Mrisho Ngassa/Farid Mussa dk79. 
   
Somalia; Mohamed Sherif, Hassan Ali Roble, Mohammed Tahlil Shidane, Aden Hussein Ibrahim, Hassan Hussein Mohamed, Daud Abdullah Hassan, Sidi Mohamed Omer, Mohamed Abdi Hayow/Mahmoud Adi Mohamed dk63, Jabril Hassan Mohamed, Mohamed saleh Hussein na Sadaq Abdulkadir Mohamed/Deki Abdullah Nur dk88. 


MAKUNDI 2013/2014.

Kundi A
KUNDI B
KUNDI C
-Kenya
-Ethiopia
-Zanzibar
-South Sudan

-Tanzania Bara
-Zambia
-Burundi
-Somalia
-Uganda
-Rwanda
-Sudan
-Eritrea

**FAHAMU: Timu mbili za Juu kila Kundi zitasonga Robo Fainali pamoja na Washindi wa Tatu wawili Bora.

RATIBA/MATOKEO.

TAREHE
NA
MECHI
KUNDI
UWANJA
SAA
Jumatano Novemba 27
1
Zanzibar 2 South Sudan 1
A
Nyayo
1400

2
Kenya 0 Ethiopia 0
A
Nyayo
1630
Alhamisi Novemba 28
3
Burundi 2 Somalia 0
B
Machakos
1400

4
Kili Stars 1 Zambia 1
B
Machakos
1600
Ijumaa Novemba 29
5
Sudan 3 Eritrea 0
C
Machakos
1400

6
Uganda 1 Rwanda 0
C
Machakos
1600
Jumamosi Novemba 30
7
Ethiopia 3 Zanzibar 1
A
Nyayo
1400

8
South Sudan 1 Kenya 3
A
Nyayo
1600
Jumapili Desemba 1
9
Somalia 0 v 1 Kili Stars
B
Nyayo
1400

10
Zambia v Burundi
B
Nyayo
1600
Jumatatu Desemba 2
11
Sudan v Rwanda
C
Machakos
1400

12
Eritrea v Uganda
C
Machakos
1600
Jumanne Desemba 3
13
South Sudan v Ethiopia
A
Machakos
1400

14
Kenya v Zanzibar
A
Machakos
1600
Jumatano Desemba 4
15
Kili Stars v Burundi
B
Nyayo
1400

16
Somalia v Zambia
B
Nyayo
1600
Alhamisi Desemba 5
17
Rwanda v Eritrea
C
Nyayo
1400

18
Uganda v Sudan
C
Nyayo
1600
Ijumaa Desemba 6

MAPUMZIKO





ROBO FAINALI



Jumamosi Desemba 7
19
C1 v B2

Mombasa
BADO

20
A1 v 3 BORA 1

Mombasa
BADO
Jumapili Desemba 8
21
B1 v 3 BORA 2

Mombasa
BADO

22
A2 v C2

Mombasa
BADO
Jumatatu Desemba 9

MAPUMZIKO



Jumanne Desemba 10

NUSU FAINALI




23
Mshindi 19 v Mshindi 20


BADO

24
Mshindi 21 v Mshindi 22


BADO
Desemba 11

MAPUMZIKO



Alhamisi Desemba 12
25
Mshindi wa Tatu


1400

26
FAINALI


1600


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad