Timu ya soka
ya CS Sfaxien ya Tunisia, Jana (Novemba 23,2013) imeutumia vyema Uwanja wa
nyumbani, Stade Olympique de Rades baada ya kuilaza mabao 2-0 Tout Puissant Mazembe ya DRC katika Fainali
ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika mjini Tunis.
Shukrani
kwao washambuliaji wa kimataifa wa Gabon, Ibrahim Didier Ndong aliyefunga bao
la kwanza dakika ya 16 na mshambuliaji wa Taha Yassine Khenissi aliyefunga la
pili dakika ya 90 na ushei wakimtungua kipa mahiri, Robert Muteba Kidiaba.
Washambuliaji
wote wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta na Thomas Emanuel Ulimwengu walianza
katika kikosi cha Mazembe pamoja na Tressor Mputu Mabi, lakini hawakuweza
kuwanusuru mabingwa mara nne Afrika na kipigo hicho.
Sfaxien,
timu pekee iliyoshinda Kombe la Shirikisho mara mbili tangu kutambulishwa kwa
mfumo mpya mwaka 2004, yenye maskani yake katika mji uliozungukwa na bahari ya
Mediterranean, Sfax sasa itahitaji sare katika mchezo wa marudiano Novemba 30,2013
au kufungwa kwa tofauti isiyozidi bao
1-0, mjini Lubumbashi,DRC ili kujinyakulia taji na kitita cha dola za
Kimarekani, 625 000.
Mshindi wa
pili atapata dola 432 000.
Mshindi pia
atamenyana na mabingwa wa Ligi ya Mabingwa, Al Ahly ya Misri kuwania taji la
Super Cup mechi itakayopigwa nchini Misri Februari 2014.






No comments:
Post a Comment