EPL 2013/2014:- Arsenal bado kileleni kwa Pointi 4 mbele, Chelsea yabonda 3 huku Liverpool ikichomoa katika Dakika za Lala Salama kwa Everton. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, November 24, 2013

EPL 2013/2014:- Arsenal bado kileleni kwa Pointi 4 mbele, Chelsea yabonda 3 huku Liverpool ikichomoa katika Dakika za Lala Salama kwa Everton.

Magoli mawili ya Mfaransa Olivier Giroud dakika ya 22 na 86 kwa penalti yametosha kuipa Arsenal ushindi wa 2-0 dhidi ya Southampton katika mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza jana Jioni (Novemba 23,2013) katika Uwanja wa Emirates.

Ushindi huo unaifanya Arsenal itimize pointi 28 baada ya kucheza mechi 12 na kuendelea kutesa kileleni, ikiizidi kwa pointi nne Liverpool iliyo katika nafasi ya pili.

Uh oh: Artur Boruc loses the ball to Olivier Giroud as the Frenchman takes advantage to score for Arsenal.

Wachezaji wa zamani wa Gunners, Robert Pires (kushoto) na Thierry Henry walikuwepo jukwani Uwanja wa Emirates leo na kushuhudia Olivier Giroud akiifungia Arsenal Bao 2, moja kila Kipindi, na Arsenal kujikita Pointi 4 mbele juu kileleni mwa Ligi Kuu England.

Nao Chelsea wakapata ushindi kwa mabao ya Frank Lampard kwa penalti dakika ya 21 na 82 na Oscar dakika ya 34 yameipa ushindi wa mabao 3-0 Chelsea dhidi ya West Ham United usiku huu katika mchezo wa Ligi Kuu ya England. 

Frank Lampard scored two goals as Chelsea comfortably beat West Ham at Upton Park and Lampard scored his first from the penalty spot after 20mins.

Forever blowing bubbles: Jose Mourinho has some fun with the West Ham bubbles.
EVERTON 3 – 3 LIVERPOOL.

Bao la Dakika ya 89 kwa kichwa cha Daniel Sturridge alietokea Benchi limewanusuru Liverpool na kupata Sare ya Bao 3-3 walipocheza Goodison Park na Mahasimu wao wakubwa katika Dabi ya Merseyside.

Mara mbili Liverpool waliongoza na mara mbili Everton wakarudisha na hatimae Romelu Lukaku kuifungia Everton Bao la 3 katika Dakika ya 82 na kuwapa matumani ya ushindi lakini Sturridge akasawazisha kwa kichwa baada ya frikiki.

Sare hii imewabakisha Liverpool Nafasi ya Pili sasa wakiwa Pointi 4 nyuma ya Arsenal .

FULHAM 1 – 2 SWANSEA CITY.

Jonjo Shelvey alitoka Benchi na kuipa Swansea ushindi wao wa kwanza katika Mechi 6 na kuiacha Fulham ikihaha mkiani.

Swansea walitangulia kufunga kwa Bao la kwanza baada ya Aaron Hughes kujifunga mwenyewe lakini Scott Parker akaisawazishia Fulham.

Kipigo hiki cha Bao 2-1 Uwanjani kwao Craven Cottage kilifanya Mashabiki wa Fulham wapige kelele wakitaka Meneja Martin Jol atimuliwe.

HULL CITY 0 – 1 CRYSTAL PALACE.

Crystal Palace, ambao leo wamepata Meneja mpya Tony Pulis atakaeanza kazi rasmi Mechi ijayo, leo wameshinda Ugenini walipoifunga Hull City Bao 1-0 licha ya kuwa Mtu 10.

Yannick Bolasie alipewa Kadi Nyekundu kwa rafu dhidi ya Jake Livermore na muda mfupi baadae Barry Bannan akafunga Bao la ushindi.

NEWCASTLE UNITED 2 – 1 NORWICH CITY.

Newcastle wamepata ushindi wao wa tatu mfululizo kwenye Ligi baada ya kuifunga Norwich City, inayoongozwa na Meneja wao wa zamani Chris Hughton,  Bao 2-1.

Newcastle walitangulia kufunga Bao 2 za Loic Remy na Yoan Gouffran huku Leroy Fer akiwapa Norwich Bao lao moja.

STOKE CITY 2 – 0  SUNDERLAND.

Stoke City wamepata ushindi wao wa kwanza katika Mechi 9 za Ligi katika hali tata baada ya kuifunga Mtu 10 Sunderland.

Stoke walifunga Bao lao la kwanza kupitia Charlie Adam lakini Sunderland walionewa sana pale Wes Brown alipopewa Kadi Nyekundu katika Dakika ya 36 kwa faulo ambayo hata hakumgusa Charlie Adam.

Bao la pili la Stoke lilifungwa na Steven Nzonzi.

LIGI KUU ENGLAND RATIBA:
Jumapili 24 Novemba,2013.

1630 Manchester City v Tottenham Hotspur
1900 Cardiff City v Manchester United

Jumatatu 25 Novemba,2013.


2300 West Bromwich Albion v Aston Villa

PREMIER LEAGUE
MATCHESHOMEAWAYGOALS
 PTSGPWONDRAWNLOSTWONDRAWNLOSTWONDRAWNLOSTGSGA
Legend: PTS: Points    WON: Games Won    DRAWN: Games Drawn    LOST: Games Lost    GP: Games Played    GS: Goals Scored    GA: Goals Allowed
1Arsenal28129125014112410
2Liverpool24127325012312413
3Chelsea FC24127325102222110
4Southampton2212642420222157
5Everton21125613302311713
6Man Utd.20116233213021813
7Tottenham201162331231196
8Newcastle20126243213031717
9Manchester City FC19116145001142812
10Swansea15124351323031716
11West Bromwich Albion14113532121411212
12Aston Villa14114252042211112
13Hull1412426321105915
14Stoke13123452311141214
15Cardiff City1211335212123915
16Norwich City11123272221051023
17West Ham1012246114132914
18Fulham10123181142041121
19Crystal Palace712219114105721
20Sunderland712219204015824


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad