|
Wanafunzi wa
shule ya msingi Kiruruma wilayani Biharamulo mkoani Kagera wakiwa katika chumba cha darasa
kilichojengwa ba Jambo Bukoba kwa kushirikiana na Wananchi wa kijiji .
|
Shirika la Jambo
bukoba lililoko mkoani Kagera leo (Novemba 27,2013) limekabidhi chumba cha darasa chenye thamani
ya shilingi milioni 7.9 kwa ajili ya
wanafunzi wa shule ya msingi Kiruruma katika
halmashauri ya wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera.
Mratibu wa
shirika hilo Bw Steven Gonzaga amesema kuwa chumba hicho kimejengwa kwa
kushirikiana na wananchi ambao wamekusanya vifaa vinavyopatikana katika
mazingira yao ambavyo thamani yake ni
zaidi ya 25%.
Bw Gonzaga
amesema kuwa shule hiyo imejengewa chumba hicho
baada ya kutaja changamoto ya wanafunzi kusongamana katika darasa moja wakati shule
hiyo ikishiriki bonanza la michezo mwaka jana mkoani Kagera.
Katika hatua
nyingine amesema kuwa Shirika hilo limetoa msaada wa kujenga baadhi ya miundombinu
ya shule tano za msingi kwenye wilaya
kadhaa mkoani humo kwa lengo la kukuza vipaji na taaluma kwa wanafunzi wa shule hizo.
Steven
Gonzaga amezitaja shule shule hizo kuwa ni Rulenge (Ngara) matundu manne ya
vyoo , Tumaini (Bukoba Manispaa) madarasa mawili na ofisi ya walimu Kalalo (Karagwe) darasa moja na Kishoju
(Muleba ) iliyotengenezewa madawati 60.
Amezitaja
shule nyingine kuwa ni Kasambya (Misenyi) ukarabati wa madarasa mawili na ofisi
ya walimu, Kiruruma (Biharamulo) ujenzi wa darasa moja na Karwoshe Bukoba (
vijijini ) ukarabati wa madarasa mawili na ofisi ya walimu.
Hata hivyo
Afisa mipango wa halamshauri ya wilaya ya Biharamulo Zabron Janga kwa niaba ya mkurugenzi wake
Nassibu Mbagga amesema licha ya kupata
msaada huo jamii haina budi kuendelea kuchangia
miundombinu inayokosekana.
“Jamii haina
budi kuchangia miradi ya maendeleo katika
kupunguza changamoto za miundombinu katika taasisi za serikali ili kuweza
kuboresha maisha ya wananchi wanaohitaji taaluma ndani na
nje ya nchi”. Alisema Janga
Aliongeza
kuwa jamii inategemea sana kupata misaada na kuzidi kuathiri watoto wao katika kupata
taaluma kwenye sekta ya elimu pamoja na
miundombinu mingine katika sekta ya afya
Maji na barabara huku ikichtumia gharama kubwa kuchangia anasa kwenye
sherehe na harusi mbalimbali.
Shirika la
Jambo Bukoba lililoko mkoani Kagera linasimamiwa na raia wa kitanzania Clemence
Mulokozi mzaliwa wa Bukoba anayeishi nchini Ujerumani.





No comments:
Post a Comment