Manchester United nusura wapate ajali kama iliyowahi kuwakumba miaka kadhaa iliyopita huko Munich. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, November 27, 2013

Manchester United nusura wapate ajali kama iliyowahi kuwakumba miaka kadhaa iliyopita huko Munich.

Manchester United jana (Novemba 26,2013) nusura wapate ajali kama iliyowahi kuwakumba miaka kadhaa iliyopita huko Munich baada ya ndege waliyopanda kusitisha zoezi la kutua mita 400 kutoka kwenye sehemu ya kutulia ndege kwenye uwanja wa Konrad Adenauer uliopo huko Cologne Ujerumani.
Ndege ya shirika la Monarch Airlines A321, namba MON 9254, ilipangwa kutua uwanjani hapo  5.30pm kwa muda wa Ujerumani, lakini rubani alilazimika kusitisha kutua kwa ndege hiyo kwa sababu kulikuwa na ndege nyingine kwenye sehemu ya kutulia.

Ndege hiyo waliyopanda United ikabidi izunguke uwanja hewani na kuja kutua dakika 10 baadae saa 5.40 pm.

Abiria mmoja katika ndege hiyo, ambayo ilikuwa na wachezaji wote wa United na maofisa wengine wa timu hiyo akiwemo CEO wa zamani wa klabu hiyo David Gill waliokuwa wakielekea kwenye mchezo wa klabu bingwa ya ulaya dhidi ya Bayer Leverkusen, alisema kwamba tukio hilo lileta hali ya kutisha miongoni mwa abiria huku akifhamika kwamba ilitolewa taarifa rasmi kwamba kulikuwa na tatizo lilokuwa likiendelea. 

Mlinzi wa United Rio Ferdinand alitweet kuhusu tukio hilo muda mfupi baada ya kutua salama akisema, 'Landed in Germany....just....I’ve only just recovered after that choppy landing!

Kwenye msafara huo hakuwemo Sir Bobby Charlton, mtu mmojawapo aliyenusurika katika ajali iliyopita ya Munich, pia hakuwemo kocha mstaafu wa timu hiyo Sir Alex Ferguson.

Pamoja na kuchelewa kutua kwa ndege hiyo huko Cologne, Moyes na mlinzi Chris Smalling walienda kwenye mkutano wa waandishi wa habari wakiwa watulivu na wasiokuwa na chembe ya wasiwasi juu ya tukio hilo. 

Usiku wa leo (Novemba 27,2013) United inacheza mechi muhimu na Leverkusen huku wakiwa wana mapengo ya wachezaji wao muhimu kama Van Persie, Carrick, Jones na Vidic.

MATOKEO YA JANA:-NOVEMBA 26,2013.

Group E

Basel 1-0 Chelsea

Steaua Bucuresti 0-0 Schalke 04

Group F

Arsenal 2-0 Marseille

Borussia Dortmund 3-1 Napoli

Group G

Zenit Petersburg 1-1 Atletico Madrid

FC Porto 1-1 Austria Wien

Group H

Ajax 2-1 Barcelona

Celtic 0-3 AC Milan

Sasa Chelsea wametinga Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya  UEFA  licha ya kufungwa Bao 1-0 na FC Basel hapo Jana(Novemba 26,2013)  huko Uswisi kwenye Mechi ya Kundi E.

Barcelona walikuwa wameshatinga Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA walifungwa Bao 2-1 na Ajax huko Amsterdam na hicho ni kipigo cha kwa kwanza kwao Msimu huu chini ya Meneja wao mpya Gerardo Martino.

Ajax sasa watasafiri kwenda Italy Mwezi ujao kucheza na AC Milan ambao Jana waliitandika Celtic 3-0 huko Scotland na Matokeo ya Mechi hii kuamua nani ataungana na Barcelona.

Katika Kundi F, Timu 3, Arsenal, Napoli na Borussia Dortmund, zina uwezo wa kupata Nafasi mbili za kutinga Raundi ya Mtoano ya Timu 16 baada Arsenal kuifunga Olympique Marseille 2-0 na Borussia Dortmund kuichapa Napoli 3-1.

Arsenal watamaliza Ugenini na Napoli na Dortmund pia wako Ugenini kucheza na Marseille ambayo imeshaaga Mashindano.



TIMU ZILIZOFUZU KUINGIA Raundi ya Mtoano ya Timu 16:
[Timu 5 Bado 11]

-Bayern Munich

-Manchester City

-Atletico Madrid
 
-Barcelona

-Chelsea
 



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad