Taswira ya Mchezo wa kilimanjaro Stars ikicheza mechi yake ya kwanza ya CECAFA Challenge Cup na timu ya Taifa ya Zambia katika mji wa Machakos na kufungana bao 1-1. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, November 29, 2013

Taswira ya Mchezo wa kilimanjaro Stars ikicheza mechi yake ya kwanza ya CECAFA Challenge Cup na timu ya Taifa ya Zambia katika mji wa Machakos na kufungana bao 1-1.

Hapa vijana wetu wa Kill Stars wakiwa katika Picha ya Pamoja Kabla ya kwanza kwa kipindi cha kwanza ya CHALENJI CUP, Jana (Novemba 28,2013) yameendelea huko Machakos, Kenya kwa Mechi mbili za Kundi B ambapo Burundi iliifunga Somalia Bao 2-0 na baadae Kilimanjaro Stars kutoka Sare Bao 1-1 na Wageni Waalikwa Zambia.

Timu ya Taifa, kilimanjaro Stars Jana (novemba 28,2013)  imecheza mechi yake ya kwanza ya CECAFA Challenge Cup  na timu ya Taifa ya Zambia katika mji wa Machakos, ambao uko takriban kilometa 60 kutoka Nairobi. Timu hizo zimefungana 1-1. Kwa ujumla mchezo ulikuwa mkali na wa kusisimua sana, Katika mechi iliyotangulia ambayo iliwakutanisha Burundi NA Somalia, Burundi iliwafunga Somalia goli 2.

Bwana shiyo Pamoja na Gavana wa Machakos wakitazama chezo kati ya kilimanjaro Stars ilipocheza mechi yake ya kwanza ya CECAFA Challenge Cup  na timu ya Taifa ya Zambia katika mji wa Machakos, ambao uko takriban kilometa 60 kutoka Nairobi.

Mtanange ukiendelea
uwanja wa
Machakos.
Aidha mashindano hayo ya CECAFA ya Nchi za Afrika Mashariki na ya Kati, CHALENJI CUP, jana (Novemba 28,2013) yameendelea huko Machakos, Kenya kwa Mechi mbili za Kundi B ambapo Burundi iliifunga Somalia Bao 2-0 na baadae Kilimanjaro Stars kutoka Sare Bao 1-1 na Wageni Waalikwa Zambia.

Kwenye Mechi ya awali Burundi waliifunga Somalia Bao 2, moja kila Kipindi, kupitia Christopher Ndwarugira Dakika ya 35 na Abdul Fiston Razak, Dakika ya 65.

Katika Mechi ya Pili, Zambia ndio walitangulia kufunga Bao kwenye Dakika ya 41 kwa kichwa cha Ronald Kampamba kufuatia krosi ya Felix Katongo.

Kipindi cha Pili, Dakika ya 60, Said Morad alisawazisha kwa Kilimanjaro Stars.


Mechi inayofuata kwa Kili Stars ni hapo Jumapili itakapocheza na Somalia.

MAKUNDI ya CECAFA Challenge Cup 2013/2014.

Kundi A
KUNDI B
KUNDI C
-Kenya
-Ethiopia
-Zanzibar
-South Sudan

-Tanzania Bara
-Zambia
-Burundi
-Somalia
-Uganda
-Rwanda
-Sudan
-Eritrea
**FAHAMU: Timu mbili za Juu kila Kundi zitasonga Robo Fainali pamoja na Washindi wa Tatu wawili Bora.
RATIBA/MATOKEO:
TAREHE
NA
MECHI
KUNDI
UWANJA
SAA
Jumatano Novemba 27
1
Zanzibar 2 South Sudan 1
A
Nyayo
1400
2
Kenya 0 Ethiopia 0
A
Nyayo
1630
Alhamisi Novemba 28
3
Burundi 2 Somalia 0
B
Machakos
1400
4
Kili Stars 1 Zambia 1
B
Machakos
1600
Ijumaa Novemba 29
5
Sudan v Eritrea
C
Machakos
1400
6
Uganda v Rwanda
C
Machakos
1600
Jumamosi Novemba 30
7
Ethiopia v Zanzibar
A
Nyayo
1400
8
South Sudan v Kenya
A
Nyayo
1600
Jumapili Desemba 1
9
Somalia v Kili Stars
B
Nyayo
1400
10
Zambia v Burundi
B
Nyayo
1600
Jumatatu Desemba 2
11
Sudan v Rwanda
C
Machakos
1400
12
Eritrea v Uganda
C
Machakos
1600
Jumanne Desemba 3
13
South Sudan v Ethiopia
A
Machakos
1400
14
Kenya v Zanzibar
A
Machakos
1600
Jumatano Desemba 4
15
Kili Stars v Burundi
B
Nyayo
1400
16
Somalia v Zambia
B
Nyayo
1600
Alhamisi Desemba 5
17
Rwanda v Eritrea
C
Nyayo
1400
18
Uganda v Sudan
C
Nyayo
1600
Ijumaa Desemba 6
MAPUMZIKO
ROBO FAINALI
Jumamosi Desemba 7
19
C1 v B2
Mombasa
BADO
20
A1 v 3 BORA 1
Mombasa
BADO
Jumapili Desemba 8
21
B1 v 3 BORA 2
Mombasa
BADO
22
A2 v C2
Mombasa
BADO
Jumatatu Desemba 9
MAPUMZIKO
Jumanne Desemba 10
NUSU FAINALI
23
Mshindi 19 v Mshindi 20
BADO
24
Mshindi 21 v Mshindi 22
BADO
Desemba 11
MAPUMZIKO
Alhamisi Desemba 12
25
Mshindi wa Tatu
1400
26
FAINALI
1600

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad