![]() |
|
|
Milio ya risasi zaidi ya kumi ilisikika eneo la Ilala
Bungoni karibu na baa maarufu ya Wazee (Club ya Wazee), watu watatu
wakiripotiwa kufariki kutokana na tukio hilo linaloelezwa kuwa
limetokana na wivu wa kimapenzi.
Mfanyabiashara
huyo wa magari, Gabriel Munisi (35), jana alijiua baada ya kumuua mtu mmoja na
kujeruhi wengine watatu jijini Dar es Salaam katika tukio linalohusishwa na
wivu wa mapenzi.
Munisi,
ambaye alikuwa mkazi wa Mwanza, aliwapiga risasi watu watatu akiwamo mchumba
wake, Christina Alfred katika Mtaa wa Bungoni Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam.
Baada ya
kumpiga risasi mchumba wake huyo na kudhania kwamba amemuua, inadaiwa kwamba
Munisi aliendelea kuwamiminia risasi watu wengine na kumuua mdogo wake
Christina, Alpha (22).
Katika tukio
hilo, Christina na mtu anayedaiwa kuwa mchumba wake mpya, Francis Shumila
wamelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kujeruhiwa. Mama yake
Christina, Helen Alfred amelazwa katika Hospitali ya Amana baada ya kujeruhiwa
pia.
Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Ilala, Marieta Minangi alisema Munisi alikutwa na bastola moja,
magazini mbili na yalikutwa maganda 14 ya risasi zilizotumika na risasi mbili
ambazo zilikuwa hazijatumika.
Tukio hili
limetokea mwezi mmoja baada ya mwandishi wa habari wa ITV, Ufoo Saro kujeruhiwa
kwa risasi na mzazi mwenzake, Anthery Mushi.
Katika tukio
hilo, Mushi alijiua baada ya kumuua mama mzazi wa Ufoo na inaaminika pia tukio
hilo lilisababishwa na masuala ya mapenzi.








No comments:
Post a Comment