![]() |
|
Watu wawili
wamefariki na wengine takriban watu 50 kukwama kwenye vifusi baada ya paa ya
jumba la maduka lililokuwa linajengwa kuporomoka nchini Afrika Kusini.
|
![]() |
|
Taswira ya
jengo lililoporomoka eneo la Tongaat Kaskazini mwa mji wa Durban nchini Afrika
Kusini na kuua watu wawili mpaka sasa. (PICHA: eNCA).
|
Watu wawili
wamepoteza maisha na wengine takribani 50 wakifukiwa kwenye vifusi baada ya paa
la jengo la maduka lililokuwa linajengwa kuporomoka eneo la Tongaat Kaskazini
mwa mji wa Durban nchini Afrika Kusini.
Watu 29
wameweza kuokolewa kutoka katika jengo hilo.
Madaktari
kutoka kampuni ya Netcare 911 walifika kutoa huduma ya kwanza katika eneo hilo
la Tongaat.
“Shughuli
hii itachukua muda mrefu. Itatuchukua muda kuwafikia wale waliokwama,” alisema
msemaji wa kampuni hiyo.
Hata hivyo
ni mapema mno kujua sababu ya kuporomoka kwa jengo hilo.
Chanzo: BBCSWAHILI
Chanzo: BBCSWAHILI








No comments:
Post a Comment