COMANDANTE’ Ronaldo apiga HETITRIKI, Ureno yaenda BRAZIL huku Ufaransa ikiweka rekodi kwa kugeuza matokeo na kufuzu. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, November 20, 2013

COMANDANTE’ Ronaldo apiga HETITRIKI, Ureno yaenda BRAZIL huku Ufaransa ikiweka rekodi kwa kugeuza matokeo na kufuzu.

Mshambuliaji  Cristiano Ronaldo jana usiku ameifungia Ureno mao matatu peke yake ikishinda 3-2 dhidi ya Sweden na kukata tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia mwakani Brazil.

Portugal's Cristiano Ronaldo celebrates scoring the opening goal.
Heads down: Ibrahimovic and his team-mates look dejected after Ronaldo's third goal.
Having his say: Ibrahimovic sends home a free-kick piledriver to hand Sweden hope.
Meeting of stars: Zlatan Ibrahimovic walks menacingly towards star of the show Ronaldo.
Ureno inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa mao 4-2 baada ya awali kushinda 1-0 wiki iliyopita nyumbani, bao pekee la Ronaldo. Zlatan Ibrahimovic alijitahidi kuisaidia timu yake jana na akafunga mabao mawili, lakini bahati haikuwa yao.

Ronaldo alifunga mabao yake katika dakika za 50, 77 na 79, wakati  Ibrahimovic alifunga dakika ya 68 na 72.
Washabiki wa Ronaldo wamempachika Jina la ‘Comandante’ kufuatia upuuzi wa Rais wa FIFA, Sepp Blatter, kumdhihaki Ronaldo na kumfananisha kama Kamanda wa Jeshi huku akimshabikia Lionel Messi.



Huko Stade de Paris, Jijini Paris, France walipindua kipigo cha 2-0 walichokipata Kiev na kuibamiza Ukraine 3-0 na wao kufuzu kwenda Brazil.

Wengine walioungana na Portugal na France ni Croatia na Greece.

MATOKEO YOTE YA MECHI ZA PILI ZA KUFUZU KOMBE LA DUNIA 2014

Sweden 2 – 3 Portugal (Agg: 2-4)
France 3 – 0 Ukraine (Agg: 3-2)
Algeria 1 – 0 Burkina Faso (Agg: 3-3)
Croatia 2 – 0 Iceland (Agg: 2-0)
Romania 1 – 1 Greece (Agg: 2-4)


TIMU AMBAZO ZIMEFUZU KWENDA BRAZIL

[Jumla 30 Bado 2]:

Afika [Nchi 5]: Nigeria, Ivory Coast, Cameroun, Ghana, Algeria.

Europe [Nchi 13]: Belgium, Bosnia-Herzegovina, England, Germany, Italy, Netherlands, Russia, Spain, Switzerland, Portugal, France, Croatia, Greece.

South America [Nchi 5, Uruguay wapo kwenye Nchujo]: Argentina, Brazil (Wenyeji), Chile, Colombia, Ecuador.

Asia [Nchi 4, Jordan wapo kwenye Mchujo]: Australia, Iran, Japan, South Korea.

North & Central America/Caribbean [Nchi 3, Mexico wapo kwenye Mchujo]: Costa Rica, Honduras, USA.

Oceania[New Zealand wapo kwenye Mchujo].

- DROO YA KUPANGA MAKUNDI:

-KUFANYIKA TAREHE 6 DESEMBA 2013 Costa do Sauípe Resort, Mata de São João, Bahia, Brazil.

-Kwenye Droo hiyo Timu 7, pamoja na BRAZIL, ambazo ziko juu kwenye Listi ya FIFA ya Ubora Duniani zitawekwa Chungu Na 1 na Timu nyingine 24 zilizobakia zitagawanywa nane nane na kuingizwa Vyungu vingine vitatu na kutenganishwa kutoka Mabara zinakotoka.

-FAINALI KUCHEZWA: 12 Juni 2014 hadi 13 Julai 2014
 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad