Baadhi ya Pembe za Tembo zilizokamatwa katika
bandari ya Malindi mjini Zanzibar jana (Novemba 13,2013) zikisubiri kuhesabiwa ili kupata idadi kamali na
thamani yake na uzito kwa ujumla.
|
Zoezi likiendelea kupekuwa makunia ya Makombe
ya Pwani kutowa magunia yaliohifadhiwa Pembe za Tembo.
|
Askari wa jeshi la Polisi wakitowa Pembe za
Tembo katika makunia wakati wa zoezi hilo jana(Novemba 13,2013) asubuhi katika bandari ya Malindi
Zanzibar.
|
Shehena
kubwa ya pembe za tembo ikiwa na vipande 1,021 na uzito wa kilo 2,915
ambayo haijawahi kukamatwa nchini imenaswa katika bandari ya Zanzibar
huku ikishuhudiwa na Mawaziri wa serikali zote mbili wakiongozwa na Waziri wa
mali asili na utalii Balozi Khamis Kagasheki.
Wakiongea na
wandishi wa habari katika bandari ya Zanzibar ,Waziri wa nchi afisi ya rais
utawala bora na idara maalum Bw. Haji Omar Kheri amesema hili ni janga kubwa la
nchi na serikali kamwe haitokubali kuona wahusika wanaanchiwa na kuahidi
sheria kufanya kazi yake ,huku kwa upande wake Waziri Kagasheki ambaye
aliwisili Zanzibar asubuhii ya Jana(Novemba 13,2013) kushuhudia shehena hiyo
amesema ni lazima mtandao utokomezwe kwani utamaliza tembo wa nchii hii na
kuipoteza rasilimali ya nchi.
Waziri
Kagasheki amesema kuwa kontena hilo lilikuwa likitokea Bandari ya Dar es Salaam na
kwamba hadi sasa haijulikani mzigo huo una thamani kiasi gani na kwamba
unasadikiwa kumilikiwa na raia wa China.
Tukio hilo
linakuja zikiwa ni wiki mbili tangu waziri huyo kukamata pembe
za ndovu 706 jijini Dar es Salaam zikimilikiwa na raia wa China.
Pembe hizo
706 ni sawa na tembo 353 waliouawa katika hifadhi za wanyamapori hapa nchini.
Wachina hao
walikamatwa katika Mtaa wa Kifaru, Mikocheni wilayani Kinondoni chini ya
operesheni iliyoongozwa na Waziri Kagasheki, ambaye aliambatana na Katibu Mkuu
wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Bw.Tarish Maimuna.
Waliokamatwa
na shehena hiyo ya pembe za ndovu ni raia watatu wa China, ambao ni Xu Fujie,Chen Jinzha
na Huang Qin wote kutoka mji wa Guandung, ambao wamefikishwa mahakamani wiki
iliyopita.
Kwa upande
wake kamishna wa jeshi la polisi Zanzibar CP Mussa Ali Mussa amesema
polisi imekamata watu wawili wazalendo na inaendelea kuwahoji na kufanya
upekuzi nje ya bandari pamoja na kwamba taarifa zinaonyesha kuwa mzigo
huo ni wa raia wa China.
Operesheni ikiendelea kuhesabu Pembe za Tembo
zilizokamatwa katika bandari ya Zanzibar wakiweka hesabu sawa kuhakikisha
hesabu iliokamilika na kupata thamani yake halisi.
|





No comments:
Post a Comment