![]() |
| Siku hizi, si kitu cha kushangaza kusikia mtu maarufu au kiongozi fulani atakuwa kwenye Facebook saa fulani kwa ajili ya kujibu maswali ya wananchi / mashabiki wake. |
Siku hizi,
katika kila watu kumi wanaotumia mtandao, basi angalau watano kati ya hao
wanatumia mitandao jamii. Kuna baadhi ya watu wamegeuza mitandao hii kuwa kama
ni sehemu ya mawasiliano, ama ya mtu kwa mtu au ya kibiashara.
Siku hizi,
si kitu cha kushangaza kusikia mtu maarufu au kiongozi fulani atakuwa kwenye
Facebook saa fulani kwa ajili ya kujibu maswali ya wananchi / mashabiki wake.
Mitandao hii ni kama vile Facebook, Twitter, Jamiiforums nk, hivyo basi,
hatuwezi kuepuka ushawishi wa mitandao jamii katika jamii yetu.
Matumizi bora
ya mitandao jamii huweza kuleta faida nzuri sana, ila huwa kinyume pale
inapotumika sivyo, ama kwa kutokujua ama kwa kuamua. Hivyo leo hii tuangalie
mambo kadhaa ya kuepuka unapotumia mitandao jamii.
1. Epuka
kujiacha wazi kwenye mitandao jamii.
Kuna baadhi
ya watu wamegeuza mitandao jamii ni dunia yao nyingine kabisa, wao kila kitu
wanachokifanya utakiona kwenye mitandao jamii, kala nini, anadate na nani,
kavaa nguo gani nk.
Mitandao jamii ni uigaji (Simulation) ya maisha ya
halisi.Tukiwa kwenye maisha halisi, sio watu wote wanaoweza kujua maisha yako
kwa undani,kwani kuna vikomo, kuanzia wale mulio nyumba moja, munaofanya kazi
pamoja nk.
Ingawa
kwenye mitandao jamii wengi wanaweza kuchunga kwa kutumia michungo ya ufaragha (Privacy
setting) lakini si wote wanaojua hilo, pia tumeona mamia ya akaunti za watu
zikivamiwa na wavamizi wa mtandao (Hackers) na kuweka hadharani taarifa zao
nyingi.
Hivyo epuka
kuweza kila kitu kwenye mitandao jamii, kula na kikomo na pia anza kuchunga
marafiki zako juu ya nani anaweza kuona nini. Unaweza kuangalia Video HAPA jinsi
ya kuchunga ufaragha kwenye Facebook.
2. Jichunge kwenye utumaji.
Je ushawahi
kusikia mtaani wanasema jamaa ana gubu (anaongea sana?), kwenye mitandao jamii
pia kuna watu wana gubu, wanachonga sanasana. Hawa ni wale watu ambao kila
dakika wametuma kitu kipya, hii sio tu hufanya kupoteza mvuto kwa
wanaokufuatilia, bali pia umuhimu wa makala zako hupungua.
Binafsi huondoa watu
aina hii kwenye mlisho wa maboresho (activities feeds) bila hata
kujiuliza.
Hivyo, ili
kuepuka kutengwa au kuonekana unachonga sana, chunga idadi ya maboresho
unayotuma kwa siku.
3.Epuka
kutuma makala za ngono, dini au siasa kama wewe si muhusika.
Hivi ni vitu
ambavyo huathiri watu wengi sana, chukulia mfano wewe ni rafiki wa bwana X,
unafungua Facebook au Twitter yako unakutana na picha ya ngono imejaa kwenye
mlisho wa maboresho toka kwa rafiki yako.
Ukweli ni kuwa utajisikia vibaya mno
ama kama na wewe ni wa aina hiyo. Hii pia ni sawa na kwa mambo ya dini na
siasa.
Nchi yetu
ikiwa ni nchi isiyo na dini, ila watu wake wamechanganyika mnomno, kwenye kila
marafiki zako wawili, kuna mmoja ni wa dini nyingine, hivyo epuka kutuma makala
za dini zinazoudhi, zenye kebehi au kuudhi wengine.
Jaribu kuwa mtu ambaye
utaweza kuishi na watu wote. Mfano huu pia tuuchukue kule uraiani, kuna baadhi
ya watu hukimbiwa, hivyo chukua tahadhari kabla ya kukimbiwa.
4.
Usihamishie hasira zako kwenye mitandao jamii.
Kuna baadhi
ya watu, wakishauziwa nyumbani, hasira zinaishia kwnye mitandao jamii,amini
usiamini, mitandao jamii haiwezi kukusaidia kutuliza hasira zako zaidi ya kukupotezea
muda na kujidhalilisha.
Ni sawa na yule mtu mwenye ugomvi na mke / mume wake
halafu anapita kila nyumba kutangazia mapungufu ya mwenza wake, jamii nzima
inajua, siku mutakaporudiana, watu wote washajua mapungufu ya mwenza wako, je
utafuta toka kwenye vichwa vyao?
Kwenye
mitandao jamii vilevile, kuna baadhi ya watu kuhifadhi kila unachotuma na siku
ya siku watatumia kuja kukashambulia. Kaa mbali na mitandao jamii kama unaona
hauwezi kuchunga mhemuko (emotion) wako.
5.Siyo
kila mtu lazima awe rafiki yako.
Chukulia
mfano mitaani tunamoishi, kuna watu wa aina mbalimbali, na siyo kila mtu ni
rafiki yako, kuna baadhi ya watu hata hautaki kuwasogelea kutokana na tabia
zao, hii ni sawa kwenye mitandao jamii.
Epuka
kukubali maombi ya urafiki toka kwa kila mtu, haswaa ambao hauwafahamu.
Marafiki sio tu huweza kutumika kujenga taswiura yako, bali kuna baadhi ya
marafiki si marafiki, hivyo chunga marafiki zako la sivyo ipo siku utakuja
kujuta.
Hayo ni
mambo muhimu kwa ajili ya afya ya utumiaji wa mitandao jamii, usisahau kulike
Kurasa yetu ya Facebook kwa makala mbalimbali za IT kila wiki https://www.facebook.com/dudumizi








No comments:
Post a Comment