![]() |
Hii ni mara ya 6 kwa Cameroun kucheza Fainali za Kombe la Dunia na mara
nyingine zikiwa Miaka ya 1982, 1990, 1994, 1998, 2002 na 2010 ambayo ni Rekodi
kwa Bara la Afrika.
|
Nchi ya CAMEROUN leo (Novemba 17,2013) huko Yaounde wameibonda Tunisia
Bao 4-1 na kuwa Nchi ya 3 toka Afrika,kufuatia Jana (Novemba 16,2013) ,Nchi ya Nigeria
na Ivory Coast kufuzu kwenda
Brazil Mwakani kucheza Fainali za Kombe la Dunia.
Katika mchezo huo Magoli ya Cameroun yamefungwa na Pierre Webo Dakika ya
4,Benjamin Moukandjo Dakika ya 30,Jean
Makoun katika dakika ya 66 & 86 huku
goli la Tunisia likifungwa na Ahmed
Akaichi dakika ya 51.
Hii ni mara ya 6 kwa Cameroun kucheza Fainali za Kombe la Dunia na mara
nyingine zikiwa Miaka ya 1982, 1990, 1994, 1998, 2002 na 2010 ambayo ni Rekodi
kwa Afrika.
Katika Mechi ya kwanza huko Tunis, Cameroun na Tunisia zilitoka Sare 0-0
lakini leo Cameroun walistahili kwa kila kitu ushindi wao kwa jinsi
walivyotawala na kudhibiti Mechi hii huku Nahodha wao Samuel Eto’o leo akiwa
mlishaji na mwongozaji mkuu.
Sasa Afrika imeshapata Timu 3 za kwenda Brazil na mbili za mwisho
zitapatikana Jumanne kwenye Mechi mbili za mwisho kati ya Algeria na Burkina
Faso na Egypt na Ghana.
![]() |
| Senegal 1 Ivory Coast 1 . |
AFRIKA RATIBA/MATOKEO:
Marudiano:-Jumamosi Novemba 16,2013.
Nigeria 2 Ethiopia 0 [Jumla ya Mabao kwa Mechi mbili 4-1]
Senegal 1 Ivory Coast 1 [Jumla ya Mabao kwa Mechi mbili 2-4]
Jumapili Novemba 17,2013.
Cameroon 4 Tunisia 1 [Jumla ya Mabao kwa Mechi mbili 4-1]
[Saa za Bongo]
[Katika Mabano Matokeo Mechi za Kwanza]
Jumanne Novemba 19,2013.
19:00 Egypt v Ghana [1-6]
21:15 Algeria v Burkina Faso [2-3]
**FAHAMU: Washindi 5 ndio watacheza Fainali za Kombe la Dunia
TIMU AMBAZO ZIMEFUZU KWENDA BRAZIL 2014.
[Jumla 24 Bado 8]:
Afika [Nchi 3 Bado 2]: Nigeria, Ivory Coast, Cameroun.
Europe [Nchi 9 Bado 4]: Belgium, Bosnia-Herzegovina, England,
Germany, Italy, Netherlands, Russia, Spain, Switzerland.
![]() |
| Nigeria 2 Ethiopia 0 . |
South America [Nchi 5, Uruguay wapo kwenye
Nchujo]: Argentina, Brazil (Wenyeji), Chile, Colombia, Ecuador.
Asia [Nchi 4, Jordan wapo kwenye Mchujo]: Australia, Iran, Japan,
South Korea.
North & Central America/Caribbean [Nchi 3, Mexico wapo kwenye
Mchujo]: Costa Rica, Honduras, USA.
**FAHAMU:
-RATIBA IMESHATOKA BOFYA HAPA: http://www.sokainbongo.com/kombe-la-dunia-brazil-2014
- DROO YA KUPANGA MAKUNDI:
-KUFANYIKA TAREHE 6 DESEMBA 2013 Costa do SauÃpe Resort, Mata de São
João, Bahia, Brazil.
-Kwenye Droo hiyo Timu 7, pamoja na BRAZIL, ambazo ziko juu kwenye Listi
ya FIFA ya Ubora Duniani zitawekwa Chungu Na 1 na Timu nyingine 24 zilizobakia
zitagawanywa nane nane na kuingizwa Vyungu vingine vitatu na kutenganishwa
kutoka Mabara zinakotoka.
-FAINALI KUCHEZWA: 12 Juni 2014 hadi 13 Julai 2014


.jpg)





No comments:
Post a Comment