Mume amuua mkewe kwa kumnyonga shingo hadi kufa kisha kufugiwa ndani kwa siku 3 na Mwanae mwenye umri wa miaka 5,Wilayani Kibondo mkoani Kigoma. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, November 21, 2013

Mume amuua mkewe kwa kumnyonga shingo hadi kufa kisha kufugiwa ndani kwa siku 3 na Mwanae mwenye umri wa miaka 5,Wilayani Kibondo mkoani Kigoma.


Mkuu wa Jeshi la Polisi wilayani Kibondo mkoani Kigoma Bw.Marko Joshua akifungua mlango katika nyumba aliyokutwa marehemu ameuawa kikatili kwa kunyongwa  shingo hadi kufa na  mumewake na mwili wake kukutwa umeharibika vibaya katika Kijiji cha Mpevyi Kata  ya Busagara Wilayani Kibondo hivi karibuni..(Picha/Habari na Kibondo Moto).


Monekano wa Mwili wa marehemu kama ulivyokutwa chumbani baada ya kuterekezwa kwa kufugiwa ndani kwa siku 3.

Picha Juu na Chini ni Mtoto aliyeishi ndani na maiti ya mama yake kwa muda wa siku tatu akiwa amebebwa na babi yake na kwamba pamoja na kukutwa akiwa hai pembeni ya marehem mama yake lakini inaonekana nae alipata suruba kiasi Fulani.

Mwanamke Mmoja Mkazi wa Kijiji cha Mpevyi Kata  ya Busagara Wilayani Kibondo ameuawa kikatili kwa kunyongwa  shingo hadi kufa na  mume wake na mwili wake kukutwa umeharibika vibaya baada ya kuterekezwa kwa kufugiwa ndani kwa siku 3, na mtoto mdogo mwenye umri wa miaka 5.
 
Taarifa za awali kutoka kamati ya Ulinzi na Usalama ya Kijiji hicho imemtaja aliyeuawa kuwa ni Bi.Anerth Shabani mwenye umri wa miaka 22, akiwa na mtoto wake Lahabu Bugaru mwenye umri wa miaka 5 ambaye amekutwa akiwa hai huku akiwa  amejeruhiwa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali sehemu za usoni na mapajani.


Baba mzazi wa kijana aliyetekeleza
mauaji  ya kikatili kwa kumnyonga 
shingo mkewe hadi kufa .
Akizungumza na kibondo moto Afisa Mtendaji wa Kijiji hicho Bw.  Felix Kabuti amesema tukio hilo limetukia usiku wa November 16 mwaka huu, Nyumbani kwake ambapo imeelezwa kuwa marehemu Anerth shabani ameuawa na mumewake shedrak yoram Chales kwa kumunyongwa kisha kuulaza mwili wake kitandani na yeye kutokomea kusikojulikana baada ya kutekeleza unyama huo.

Naye Diwani wa Kata ya Busagara Bw. Godwin Sibanilo amesema awali alipata taarifa kutoka kwa wananchi iliyoashilia kuwepo kwa harufu kali kutoka katika nyumba hiyo ambapo kwa kushirikiana na viongozi walifanikiwa kubomoa mlango na kuingia ndani ambapo walikuta mwili wa mwananke huyo na mtoto Lahabu bugaru aliyekuwa ameulalia mwili wa mama yake.

Ndugu wa mwanamke huyo aliyenyongwa waliruhusu daktari kufanya uchunguzi wa kifo hicho kimesababishwa na nini ambapo pia waliruhusu askari kufanya uchunguzi wao lakini wamegomea mwili huo kuzikwa kwa madai kuwa mwanaume huyo hakuwa ametoa mahali wakati alipomuoa binti ya.

1 comment:

  1. Dah, naona sasa wanaume wameamua kufanya yao, Serikali isipocmama imara wadada wataogopa ndoa. Huu ni zaidi ya unyama kk makonda, then hili eneo nalifhm vema coz ndiko niliko anzia kazi

    ReplyDelete

Post Bottom Ad