Michuano ya
Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (Cecafa)
ya Chalenji, inaanza kutimua vumbi wiki ijayo ikishirikisha timu 12.
Michuano
hiyo inafanyika nchini Nairobi nchini Kenya huku Tanzania yenye timu mbili
ikiwa miongoni mwa washiriki.
Katika
kuhakikisha michuano hiyo inakuwa na msisimko huku waandaaji wameialika Taifa
ya Zambia kwenye michuano hiyo.
Tanzania
itawakilishwa na Taifa ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars na Zanzibar
(Zanzibar Heroes), timu hizo tayari zipo kambini zikiajiandaa kwa ajili ya
michuano hiyo.
Kilimanjaro
Stars, ipo kundi B imepangwa katika kundi moja na timu za Burundi, Zambia na
Somalia.
Zanzibar iko
kundi (A)pamoja na wenyeji Kenya, Ethiopia, Sudani Kusini.
Aidha Kocha Mkuu wa Kilimanjaro Stars, Kim Poulsen
ametaja kikosi cha wachezaji 23 watakaoshiriki michuano ya Kombe la Chalenji
inayofanyika nchini Kenya kuanzia Novemba 27 mwaka huu.
Kilimanjaro Stars iliyotwaa kombe hilo mara ya mwisho mwaka 2010 chini
ya Kocha Jan Poulsen, na ambayo imepangwa kundi B katika michuano ya mwaka huu
itacheza mechi yake ya kwanza Novemba 28 mwaka dhidi ya Zambia kwenye Uwanja wa
Machakos.
Wachezaji wanaounda kikosi hicho cha Tanzania Bara ni makipa Deogratius
Munishi (Yanga), Ivo Mapunda (Gor Mahia, Kenya) na Aishi Manula (Azam). Mabeki
ni Erasto Nyoni (Azam), Himid Mao (Azam), Ismail Gambo (Azam), Kelvin Yondani
(Yanga), Michael Pius (Ruvu Shooting) na Said Moradi (Azam).
Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Athuman Idd (Yanga), Frank Domayo
(Yanga), Haruna Chanongo (Simba), Hassan Dilunga (Ruvu Shooting), Ramadhan
Singano (Simba) na Salum Abubakar (Azam).
Safu ya ushambuliaji inaundwa na Elias Maguli (Ruvu Shooting), Faridi
Musa (Azam), Joseph Kimwaga (Azam), Juma Liuzio (Mtibwa Sugar), Mbwana Samata
(TP Mazembe, DRC), Mrisho Ngasa (Yanga) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC).
Kilimanjaro Stars inatarajia kuondoka Jumatatu (Novemba 25 mwaka huu)
kwenda Nairobi kushiriki michuano hiyo itakayoanza Novemba 27 mwaka huu na
kumalizika Desemba 13 mwaka huu.
Kikubwa
kwetu Watanzania ni kuziombea dua timu hizo mbili ziweze kufanya vizuri,
ikiwezekana kupata ushindi wa kwanza na wa pili.
Bingwa
Mtetezi wa Chalenji Cup ni Uganda ambao walitwaa Kombe Mwaka Jana lilipochezwa
Nchini kwao kwa kuifunga Kenya Bao 2-1 katika Fainali.






No comments:
Post a Comment