|
Monekano wa
Mwili wa marehemu kama ulivyokutwa chumbani baada ya kuterekezwa kwa kufugiwa
ndani kwa siku 3.
|
Mwanamke
Mmoja Mkazi wa Kijiji cha Mpevyi Kata ya
Busagara Wilayani Kibondo ameuawa kikatili kwa kunyongwa shingo hadi kufa na mume wake na mwili wake kukutwa umeharibika
vibaya baada ya kuterekezwa kwa kufugiwa ndani kwa siku 3, na mtoto mdogo
mwenye umri wa miaka 5.
Taarifa za
awali kutoka kamati ya Ulinzi na Usalama ya Kijiji hicho imemtaja aliyeuawa
kuwa ni Bi.Anerth Shabani mwenye umri wa miaka 22, akiwa na mtoto wake Lahabu
Bugaru mwenye umri wa miaka 5 ambaye amekutwa akiwa hai huku akiwa amejeruhiwa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha
kali sehemu za usoni na mapajani.
|
Baba mzazi
wa kijana aliyetekeleza
mauaji ya kikatili kwa kumnyonga
shingo mkewe
hadi kufa .
|
Akizungumza
na kibondo moto Afisa Mtendaji wa Kijiji hicho Bw. Felix Kabuti amesema tukio hilo limetukia
usiku wa November 16 mwaka huu, Nyumbani kwake ambapo imeelezwa kuwa marehemu
Anerth shabani ameuawa na mumewake shedrak yoram Chales kwa kumunyongwa kisha
kuulaza mwili wake kitandani na yeye kutokomea kusikojulikana baada ya
kutekeleza unyama huo.
Naye Diwani
wa Kata ya Busagara Bw. Godwin Sibanilo amesema awali alipata taarifa kutoka
kwa wananchi iliyoashilia kuwepo kwa harufu kali kutoka katika nyumba hiyo
ambapo kwa kushirikiana na viongozi walifanikiwa kubomoa mlango na kuingia
ndani ambapo walikuta mwili wa mwananke huyo na mtoto Lahabu bugaru aliyekuwa
ameulalia mwili wa mama yake.
Ndugu wa
mwanamke huyo aliyenyongwa waliruhusu daktari kufanya uchunguzi wa kifo hicho
kimesababishwa na nini ambapo pia waliruhusu askari kufanya uchunguzi wao
lakini wamegomea mwili huo kuzikwa kwa madai kuwa mwanaume huyo hakuwa ametoa
mahali wakati alipomuoa binti ya.






Dah, naona sasa wanaume wameamua kufanya yao, Serikali isipocmama imara wadada wataogopa ndoa. Huu ni zaidi ya unyama kk makonda, then hili eneo nalifhm vema coz ndiko niliko anzia kazi
ReplyDelete