Timu ya soka ya Taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes leo(Novemba 27,2013)
imeanza vizuri michuano ya Kombe la
Chalenji baada ya kuichapa Sudan Kusini
kwa mabao 2-1.
Zanzibar Heroes imeshinda mechi yake hiyo ya ufunguzi dhidi ya Sudan
Kusini kwenye Uwanja wa Nyayo jijini Nairobi, leo.
Mechi hiyo ilikuwa nzuri na Zanzibar wakitawala zaidi na kama wangekuwa
makini basi wangeweza kushinda mabao mengi zaidi.
Zanzibar ndio walitangulia
kufunga mabao yote mawili kabla ya Sudan Kusini kupata la kufutia machozi.
Nao wenyeji wa Mashindano hayo, Kenya, Harambee Stars wameanza vibaya
Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge baada ya
kulazimishwa sare ya bila kufungana na Ethiopia katika mchezo wa Kundi A,
Uwanja wa Nyayo, Nairobi, Kenya.
Matokeo hayo yanaifanya Zanzibar iliyoshinda 2-1 mchezo wake wa kwanza dhidi ya Sudan Kusini iongoze Kundi na kujiweka katika mazingira mazuri ya kuingia Robo Fainali.
Ethiopia waliitesa Kenya kwa soka ya ‘Kibarcelona’, huku wachezaji wa Harambee wakitumia nguvu zaidi na maarifa haba.
Allan Wanga alijaribu sana kuisumbua ngome ya Ethiopia, lakini bahati
haikuwa yake jioni ya leo.
Kocha wa Kenya, Adel Amrouche Mbelgiji mwenye asili ya Algeria, hakuwepo kwenye benchi leo kuiongoza timu yake na habari zinasema amekerwa na kitendo cha wachezaji wake kutopewa posho kwa muda wote wa kuwa kambini kujiandaa na mashindano.
Chalenji ya msimu huu inatazamiwa kuwa na mvuto wa aina yake kutokana
na vikosi vilivyosukwa ingawa sekretarieti ya Cecafa imeonyesha wasiwasi
kutokana na mashabiki wa hapa kutokuwa na tabia ya kuhudhuria viwanjani.
Kesho (Novemba 28,2013) Kilimanjaro Stars iliyoko Kundi B, itacheza
mechi yake ya kwanza Alhamisi kwa kuikabili Zambia jioni kwenye Uwanja wa
Kenyatta mjini Machakos.
Mbali na mechi ya Stars mchezo mwingine wa kundi hilo utakuwa baina ya
Burundi na Somalia mjini humo.
Stars, Uganda, Kenya na Ethiopia ndiyo timu zinazozungumzwa zaidi mjini
Nairobi kutokana na uimara wake.
Pia mchezo wa kesho baina ya Kilimanjaro Stars na Zambia unatarajiwa
kuwa na upinzani mkali kutokana na historia ya timu hizo mbili katika michuano
hiyo.
MAKUNDI:
Kundi A
|
KUNDI B
|
KUNDI C
|
-Kenya
-Ethiopia
-Zanzibar
-South Sudan
|
-Tanzania Bara
-Zambia
-Burundi
-Somalia
|
-Uganda
-Rwanda
-Sudan
-Eritrea
|
**FAHAMU: Timu mbili za Juu kila Kundi zitasonga Robo Fainali pamoja na Washindi wa Tatu wawili Bora.
RATIBA:
TAREHE
|
NA
|
MECHI
|
KUNDI
|
UWANJA
|
SAA
|
Jumatano Novemba 27
|
1
|
Zanzibar v South Sudan
|
A
|
Nyayo
|
1400
|
2
|
Kenya v Ethiopia
|
A
|
Nyayo
|
1630
| |
Alhamisi Novemba 28
|
3
|
Burundi v Somalia
|
B
|
Machakos
|
1400
|
4
|
Tanzania Bara v Zambia
|
B
|
Machakos
|
1600
| |
Ijumaa Novemba 29
|
5
|
Sudan v Eritrea
|
C
|
Machakos
|
1400
|
6
|
Uganda v Rwanda
|
C
|
Machakos
|
1600
| |
Jumamosi Novemba 30
|
7
|
Ethiopia v Zanzibar
|
A
|
Nyayo
|
1400
|
8
|
South Sudan v Kenya
|
A
|
Nyayo
|
1600
| |
Jumapili Desemba 1
|
9
|
Somalia v Tanzania
|
B
|
Nyayo
|
1400
|
10
|
Zambia v Burundi
|
B
|
Nyayo
|
1600
| |
Jumatatu Desemba 2
|
11
|
Sudan v Rwanda
|
C
|
Machakos
|
1400
|
12
|
Eritrea v Uganda
|
C
|
Machakos
|
1600
| |
Jumanne Desemba 3
|
13
|
South Sudan v Ethiopia
|
A
|
Machakos
|
1400
|
14
|
Kenya v Zanzibar
|
A
|
Machakos
|
1600
| |
Jumatano Desemba 4
|
15
|
Tanzania v Burundi
|
B
|
Nyayo
|
1400
|
16
|
Somalia v Zambia
|
B
|
Nyayo
|
1600
| |
Alhamisi Desemba 5
|
17
|
Rwanda v Eritrea
|
C
|
Nyayo
|
1400
|
18
|
Uganda v Sudan
|
C
|
Nyayo
|
1600
| |
Ijumaa Desemba 6
|
MAPUMZIKO
| ||||
ROBO FAINALI
| |||||
Jumamosi Desemba 7
|
19
|
C1 v B2
|
Mombasa
|
BADO
| |
20
|
A1 v 3 BORA 1
|
Mombasa
|
BADO
| ||
Jumapili Desemba 8
|
21
|
B1 v 3 BORA 2
|
Mombasa
|
BADO
| |
22
|
A2 v C2
|
Mombasa
|
BADO
| ||
Jumatatu Desemba 9
|
MAPUMZIKO
| ||||
Jumanne Desemba 10
|
NUSU FAINALI
| ||||
23
|
Mshindi 19 v Mshindi 20
|
BADO
| |||
24
|
Mshindi 21 v Mshindi 22
|
BADO
| |||
Desemba 11
|
MAPUMZIKO
| ||||
Alhamisi Desemba 12
|
25
|
Mshindi wa Tatu
|
1400
| ||
26
|
FAINALI
|
1600
|





No comments:
Post a Comment